Tumia Nguvu ya ubongo wako kua Tajiri.

By | July 16, 2016

Ubongo wako ndio chanzo cha kila kitu kwenye maisha yako.
Unavyopanga kichwani ndio itakavyotokea kwenye matendo.

Ukijiona huwezi kumiliki gari kuanzia kwenye akili yako ukaanza kuona gari lilivyo ghali huwezi kuweka matendo ya kupata gari. Tengeneza ubongo wako ukuletee mawazo ambayo yatabadilisha vitendo vyako.

Usiishie kutaka kua tajiri. Panga kua tajiri na fanya vitendo vya kua tajiri. Daudi aliweza kupambana na simba kutokana na alivyokua amejitengenezea mawazo ya kijasiri na kuondoa woga wote.

Simba wako wewe leo ni nini. Ni kitu gani unachokihofia kwenye maisha. Unakiona ni kikubwa sana wewe hukistahili? Badilisha mawazo yako leo Maisha yako yatabadilika.

Weka mpango wa kua tajiri leo inawezekana anza kubadili fikra zako kwanza. Changamoto kubwa uliyonayo ni woga juu yako mwenyewe pale unapojihisi kua hutaweza hii itakutesa sana kama utashindwa kuiondoa.

Kabla hujawaza utakuaje tajiri anza kuwaza kwanini! Kwanini uwe tajiri? Kwanini uwe na uhuru wa kifedha? Kwanini matatizo ya pesa yasiwe matatizo tena kwako?  Ukishapata majibu ndio utaweza kujua unaweza kua tajiri.

Penye nia pana njia. Kile kinachokufanya wewe utamani kua na utajiri ndio nia yenyewe usirudi nyuma.

Ukiwa tajiri utaweza kujisadia mwenyewe na wahitaji wengine.
Hakuna kitu utakachokitaka kinachohitaji pesa ukikose.
Utaweza kujitolea sehemu mbalimbali.
Utaweza kuwasaidia maskini.
Utaweza kutatatua matatizo yote ya kifedha.
Yako mambo mengi sana utaweza kuyafanya Ukiwa tajiri.

Anza leo hakuna kisichowezekana. Maisha yako ni yako. Chukua hatua ya kuyabadili.

Karibu sana
#JacobInspirationalTeachings2016
#Contact +255654726668

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *