“Wote tumezaliwa duniani ili kuifanya dunia kua bora. Kuitoa pale tulipoikuta na kuipeleke sehemu nyingine nzuri Zaidi.”
Kila binadamu ana uwezo wa kipekee sana ndani yake na ana nguvu kubwa sana ndani yake vyote hivi tumezaliwa navyo. Tumeanza kuvigundua kidogo kidogo kadiri tunavyojifunza kila siku. Tumezaliwa na zawadi nyingi sana ndani yetu ambazo tunatakiwa tuziache hapa duniani tuzitumie hapa duniani. Embu jiulize aliepewa uwezo wa kugundua Computer angekaa nao tu kimya dunia ingekua wapi leo? Tunaona watu wenye ubunifu wa namna mbalimbali kwenye vitu kila siku na wewe ni wakati wako kujua ni sehemu gani una uwezo wa kuvumbua. Sio lazima uje na kitu kipya kabisa unaweza kuendeleza vya wengine ukavifanya vikawa bora Zaidi ya walivyo acha. Dunia inakuhitaji sana usikubali uondoke hivi hivi hujafanya uvumbuzi wa aina yeyote yaani uondoke duniani ukiwa hujaacha kitu chochote cha pekee? Wewe ni wa pekee na una vitu vya kipekee ndani yako usikubali kuondoka navyo duniani. Hivyo vitu vya pekee ndio vinakupa nafasi ya wewe kubakia duniani hadi leo.
Nakupa siri hii ya kuvumbua ili uweze kufanya mambo makubwa kupitia siri hii utaweza kutengeneza historia mpya utaweza kuacha alama kubwa sana duniani. Usikubali kuishia kua mtumiaji wa kila kitu kinachokuja peke yake jaribu na wewe kuvumbua vitu wengine watumie vya kwako. Tumia ubunifu wa kipekee ulioko ndani yako kutengeneza dunia ambayo itakua na manufaa kwako na kwa wengine. Mungu alikuumba ukiwa mkamilifu umejaa kila aina ya zana ndani ya kichwa chako. Ukija kwenye mazingira uliyonayo umezungukwa na vitu vingi sana ambayo unaweza kuvitumia na ukaifanya dunia ikawa bora sana. Na hapa dunia haiwi bora tu watu hawafurahii tu kile ulichovumbua bali maisha yako yatakua bora sana kwasababu umeongeza thamani kwenye dunia.
Learning and innovation go hand in hand. The arrogance of success is to think that what you did yesterday will be sufficient for tomorrow. William Pollard
Ili uweze kuvumbua unahitaji kujifunza sana. Kuzaliwa na uwezo wa kipekee ndani yako haimaanisha wewe unaweza kila kitu lazima ukubali kujifunza kuutumia uwezo ulioko ndani yako. Hata kama una kipaji kizuri sana cha uimbaji ili uweze kufanya vizuri Zaidi unahitaji ukubali kujifunza sana ili uwe bora Zaidi. Mafanikio yako ya jana achana nayo ndio maana hapa tunazungumzia siri za kuwa hai leo na sio jana wala kesho. Mafanikio yako ya jana yanaweza kua sababu ya kukushusha wewe hadi chini ukawa wa kawaida sana. Ulichokivumbua jana tayari kimepita wewe kua hai leo ni nafasi ya kuvumbua kingine bora Zaidi.
Innovation is the only way to win. – Steve Jobs
Ili uweze kua mshindi lazima ukubali kua mvumbuzi tuanelewe kwamba wewe ni mshindi tangu umezaliwa hadi sasa lakini ili uweze kwenda hatua nyingine na kubwa Zaidi lazima ukubali kua mvumbuzi. Kwenye chochote unachokifanya kubali kuwa mbunifu. Ili uwe bora Zaidi na Zaidi lazima ukubali kuwa mvumbuzi.
Kuna mabilioni ya vitu vipya vinavumbuliwa kila siku na wanadamu wenzako na kuifanya dunia kua bora na mahali pazuri kwa kuendelea kuishi ni wakati wako wa wewe kujua upo kwenye nafasi gani na uitumie vyema ili kuvumbua vitu vipya katika dunia hii.
Jacob Mushi
Siri 7 za Kua Hai Leo
0654726668
jacob@jacobmushi.com