Habari za leo Rafiki yetu mpendwa. Ni matumaini yangu kwamba umeanza vyema siku kuu yak o leo. Sisi kwa pamoja kama uongozi wa USIISHIE NJIANI tunakutakia siku kuu njema.

Ujumbe kutoka kwa Mwalimu Jacob Mushi

”Kwenye siku kuu hizi pamoja na kufurahi sana kile ambacho umekifanya kwa mwaka mzima unatakiwa pia uutumie muda huu kutafakari juu ya safari yako hapa duniani. Jitazame ulipotoka, ulipo, na unapokwenda tazama lile kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.

Ni kweli bado upo kwenye mstari au umeshapotea?

Unavyovifanya sasa hivi vinatoa picha ya kule unapoelekea? Sio kwa watu wengine ila kwako mwenyewe?

Kitu cha kushangaza ni kwamba kuna wengi sana ambao wameshasahau kama wana safari. Na bahati mbaya sana ukijisahau kama unasafiri utakuja kujikuta umeelekea katika njia ambayo sio. Kazi itakuja kuwa kubwa sana kuanza kuitafuta tena ile njia yako.

Kipindi hiki ndio unapaswa pia kuyatafakari maono yako makubwa. Je ni kweli umeamua kwenda kuyatimiza? Au wewe mwenyewe umeshaanza kujikatia tamaa.

Pamoja na raha zote unazopata njiani usije kusahau unapokwenda. Ndio maana ni muhimu sana kupata muda wa kutafakari juu ya safari yako.

Watu wengi wameingia kwenye mtego huu wa kujisahau kwamba wanasafiri baada ya kukutana na raha kidogo njiani. Kumbe baada ya raha kuna hatua nyingine unapaswa kupiga.

Usiishie njiani songa mbele mafanikio ni lazima.

Furaha yangu kubwa ni kuona wewe unafanikiwa.”

Jacob Mushi

Tunakutakia Heri ya ChristMass na mwaka Mpya. Nunua vitabu kwenye mtandao huu ujisomee kipindi hiki cha siku kuu.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading