Uchaguzi.

Neno Uchaguzi linamaanisha vitu vingi lakini mimi nitazungumzia Uchaguzi wa vitu au Uchaguzi bora katika kuelekea maisha yenye mafanikio.

Siku zote kwenye Uchaguzi ili uweze kuchagua kitu kilicho bora lazima vile unavyovichagua viwe vichache.
Vikiwa vichache itakusaidia wewe kufikiri vyema na kufanya maamuzi sahihi.

Mara nyingi kukiwa na vitu vingi vya kuchagua kunatakiwa kuwe na mchujo hadi vibaki vile vilivyo bora pekee. Hapi ndipo Uchaguzi wako utanoga na utaweza kuchagua vyema lazima kuwe na vigezo muhimu ili uweze kuchuja.

Tuseme umeenda sokoni kununua machungwa unataka machungwa mawili tu yaliyo bora. Lakini upo kwenye meza yenye machungwa 500 kiukweli na hakika huwezi kupata chungwa bora kwenye machungwa 500 na hata Uchaguzi wako utakua wa  mashaka. Lakini yanapokua machungwa 10 wewe kupata bora ni rahisi sana na wala hutababaika.

Angalia sana wakati unafanya Uchaguzi wa vitu kwenye maisha yako. Usijikute unaingia kwenye kundi kubwa lazima uwe na mchujo uwe na vigezo.

Wakati unachagua marafiki lazima uwe na mchujo lazima uwe na vigezo. Ukiona wewe una marafiki wengi upo katika hatari ya kupotea. Ukiona wewe kila mtu anaweza kua rafiki yako kupotea ni rahisi sana.

 Mtu yeyote  anaetamani kua mtu mkuu hua haambatani na kila mtu na wakati wa kufanya Uchaguzi anakua makini sana. Watu wakuu siku zote sio marafiki wa kila mtu wala hawaongeo hovyo. Hawajichanganyi hovyo.

Ukiona makundi uliyonayo hayakusaidii kwa chochote katika kukufanikisha kwenye ndoto zako kimbia haraka. Umekaa na mtu siku nzima haongeo lolote la kukujenga kimbia haraka kafanye Uchaguzi upya.

Ni bora kukaa peke yako kuliko kukaa na marafiki waovu.

Kua makini sana unapofanya Uchaguzi hasa wa marafiki.

Karibu sana.

Mwandishi: Jacob Mushi
0654726668

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading