Vijana ndio tegemeo kubwa katika sehemu mbalimbali za kijamii, kidini, n ahata pia kisiasa. Kwenye serikali tuna maaskari polisi wengi ambao ni vijana pamoja na wanajeshi. Dini zetu pia zinahitaji vijana Zaidi kwasababu ndio pekee wenye nguvu kuliko wazee na watoto. Vijana pekee ndio wanaweza kufanya mambo makubwa na yakaleta matokeo makubwa.

Vijana ndio wanahusika Zaidi kwenye matukio maovu duniani.

Vijana ndio wameajiriwa Zaidi kwenye makampuni kuliko wazee vijana ndio wanaofanya kazi kubwa kuliko wazee.

Kwenye siasa vijana ndio wanatumika Zaidi kwasababu wao wana nguvu na pia wanahamasika haraka Zaidi.

Sasa wewe kijana mwenzangu umeona kila mahali watu wanataka nguvu zako. Kila sekta inakuhitaji wewe ili uweze kuweka nguvu zako. Naomba ujiulize je wewe mwenyewe unajihitaji kwa kiasi kikubwa kama ambavyo watu wanatamani nguvu zako?

Soma: BARUA MAALUMU KWA VIJANA AMBAO HAWAJAOA AU KUOLEWA

Maono yako yanakuhitaji wewe kijana, watoto wako ambao umeshawazaa na ambao bado wanahitaji nguvu zako.

Mke wako, mme wako anazihitaji nguvu zako sana.

Kila upande unahitaji nguvu zako.

Kosa moja ambalo unaweza kulifanya ni kufanya hayo yote bila kujua unapokwenda, bila ya kutambua unataka kuja kuwa nani.

Nguvu zako zitakuwa zinapotea bure kama hujui unataka kuja kuwa nani, na ni wapi unaelekea. Utajikuta unafanya kila linalotokea kwasababu tu una nguvu.

Nikuombe kitu kimoja kijana mwenzangu, sio vibaya kufanya kazi huko na huko, lakini ni hatari sana unapofanya ukiwa hujui mwelekeo wa maisha yako.

Msingi wa kwanza ambao unapaswa kuupata wewe kama kijana ni kujua kwanini upo hapa duniani.

Tambua unataka kuwa nani?

Unataka jamii na dunia ikutambue wewe kama nani?

Ukishatambua hayo hapo sasa utaweza kutambua ni wapi unapaswa kupeleka nguvu zako Zaidi.

Utapata nafasi ya kufanya uchaguzi sio kila linalokuja linakubeba tu kwasababu upo upo.

Tafuta kujua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.

Usiishi kwa mkumbo muda unakwenda, ukiwa mzee utakuja kueleza nini kwa wajukuu zako?

Anza sasa, jua kusudi lako mapema ukiwa kijana na uanze kulifanyia kazi.

Nakushauri Usome vitabu viwili nilivyoandika UMUHIMU WA MAONO na SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO vitakusaidia sana kupata mwelekeo wa maisha yako. Unaweza kuvipata kwenye maelezo mwishoni mwa Makala hii.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading