Habari ndugu msomaji natumaini u mzima wa afya na karibu sana.  Leo tunaendelea kujifunza pamoja topic ya leo inasema asikudanganye kua muda bado upo. Maisha ya sasa yamekua mafupi sana watu wanapoteza maisha kila siku tunabaki kujiuliza lini itakua ni mimi. Leo ninakwenda kukueleza kua acha sasa kujiuliza lini utaondoka bali anza kufanya maandalizi ya kuondoka.
Kama tunavyojua hatutaondoka na kitu hapa duniani mandalizi yetu tunayoyafanya ni kuacha vitu hapa duniani. Embu jiulize leo umekwenda ni nani atalia? nani utamgusa? na utamgusa kwa lipi? Je watalia tu kwa sababu umeondoka ukiwa kijana mdogo? Watalia kwa sababu ulikufa kifo kibaya? Watalia kwa kua umeacha mume/mke na watoto wadogo?
Ukiweza kujua kwamba watalia kwa sababu gani sasa ni wakati wako na wangu kuongeza vitu vya kuacha hapa duniani. Jiulize tena ukiondoka leo familia yako utakua umeiachia nini? Jamii iliyokuzunguka utakua umeaicha nini? Nchi yako utakua umeiachia nini? Sio lazima uwe kiongozi tu hivyo ulivyo umeshafanya nini katika dunia hii? Ukiondoka leo utaacha alama gani duniani? Sio wakati wa kujilaumu ni wakati wa kufanya. Unaweza ukasema sina pesa. Sina kazi. Sina chochote. Sio lazima uwe na kitu wewe tayari ni kitu cha kwanza kukitumia kuanza kuacha alama duniani.
Onyesha upendo kwa kila binadamu aliekuzunguka unaekutana nae popote. Mshukuru Mungu kwa watu wazuri ulio nao huku duniani. Baraka za Mungu zitakujilia kwenye kila unalolifanya.
“Leo ndio yako, jana imepita, kesho huijui” jiulize utaacha jambo gani jema kwenye maisha ya watu la kuwainua. Ukiondoka utakumbukwa kwa kila ulilolifanya kwenye maisha ya watu. Kama ni baya litakumbukwa pia jitahidi utende wema onyesha upendo kwa kila mtu. Achana na chuki hazitakusaidia kama kuna mtu unamchukia muonyeshe upendo leo. Kama kuna mtu ulikua una kisasi nae mpigie simu leo muweke mambo sawa.
Mtu asikwambie kua wewe bado mdogo subiri kwanza. Ni wakati wako huu wa kufanya kila linalowezekana kufanywa kwa umri wako ukiondoka uwe umeacha alama hapa duniani.  Kuna wakati jiulize pia siku ukiondoka vitu ulivyokua unavifanya kwa siri vitakua wazi.
Jambo la msingi la kufanya jitahidi kuacha alama kwenye hii dunia acha kuwalaumu watu. Ni wakati wako sasa. 
Asante sana kwa kusoma natumaini umejifunza vitu leo.
Imeandikwa na Jacob Mushi
Karibu sana 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading