Inawezekana umekuwa na fikra hizi potofu kwamba ukiishi duniani maisha yenye dhiki, machozi na mateso kila siku basi utakwenda kuishi Maisha ya raha kule mbinguni. Ukweli ni kwamba kama umeshindwa kuishi kwa furaha hapa duniani unaweza kujuta Zaidi huko unapokwenda.

Sio vibaya kutazamia mazuri kule tunapokwenda lakini ni muhimu kutambua thamani ya Maisha yetu hapa duniani. Wewe hukuzaliwa uje uteseke hapa duniani.
Vitu vyote ambavyo vimeumbwa na Mungu unapaswa kuvifurahia lakini tu usije ukamsahau Mungu wako. Jukumu lako wewe ni kukaa na Mungu akuonyeshe kusudi lake kwenye Maisha yako hapa duniani.

Mungu hajakusudia uishi Maisha ya mateso, ulie kila siku, upatwe na mabaya kila wakati. Hayo yanaweza kutokea kwasababu maalumu lakini hayo sio Maisha yako.
Unapaswa kuishi vizuri hapa duniani ili uje kuishi vizuri Zaidi kule unapokwenda. Kama utashindwa kuishi vizuri hapa kule unapokwenda utaishi Maisha ya majuto. Ukishindwa kuutumia muda wako hapa duniani vizuri utajikuta umeupoteza kwa kufanya mambo yasiyo kusudiwa.

Usimlaumu Mungu kwa matatizo yako. Kuna mambo ambayo yanamhusu Mungu moja kwa moja na mengine unapaswa kuyafanya wewe. Kwasababu hajakupa akili ya bure, hajakupa marafiki wa bure, hajaweka watu ambao unaweza kuwatumia ukapata fedha bure. Mungu anahusika pale tu uwezo wako unapofika mwisho.

Kiwango cha baraka unazopokea kinaendana kabisa na kiwango cha ufahamu wako. Huwezi kupokea kilichokuzidi kwasababu utashindwa kudhibiti na mwisho wake utamkosea Mungu. Kile unachokiona kama kinaendana na uwezo wa ufahamu wako ndio utapewa.

Ukiomba gari na Mungu anaona kabisa wewe huwezi kumiliki gari kwasababu utapotea kwenye dhambi hutakaa upate gari hadi ubadilike.
Matokeo yeyote ya nje yanatokana na matokeo ya ndani. Unapobadilika ndani ndipo na nje kunabadilika.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading