Home » USIISHIE NJIANI » Ukiweza Kupiga hatua hii maisha yako hayatakua ya kawaida.

Ukiweza Kupiga hatua hii maisha yako hayatakua ya kawaida.


Katika maisha vipo vitu vingi tunatafuta kila siku. Kwa ajili ya kujifurahisha ni pia kwa malengo tuliyojiwekea.  Kuna hatua ambazo ukizifikia maisha yako yanakua ni ya tofauti na wengine. Pale ambapo changamoto zilizokua zinakupa hofu sana ukaweza kuzivuka. Vile vitu ulivyokua unaogopa sana kuvifanya ukivifanya maisha yako yanakua sio ya kawaida tena. Unakua umepiga hatua nyingine zaidi.  

Embu tazama leo ukizifikia zile ndoto zako kubwa na kuanza kuishi maisha hayo maisha yako yatakuaje? Usikate tamaa haraka hivyo bado safari ni ndefu usijiangalie leo huna nini bali angalia uzuri wa ndoto zako.

Dunia ina kila kitu ambacho wewe unakihitaji ni wewe kutokata tamaa na kuendelea kupambania maono yako na ndoto zako. 

Ione kila siku ni zawadi toka kwa Mungu na uitumie vyema kutimiza kile alichoweka ndani yako. Mungu ana sababu kubwa sana ya kukuweka hai siku ya leo. Anatarajia uanze kufanya vitu vya tofauti. 

Anza leo kubadilisha maisha yako.
Ukitaka kutoka hapo ulipo anza kufanya vile vitu ulivyokua unavihofia sana. Anza kufanya vile vitu ulivyokua unaona ni vigumu.

Maisha yako hayatakua kama yalivyokua.

#JacobInspirationalTeachings
#Contact +255654726668
www.mushijacob.blogspot.com

About

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: