Mwanadamu anaongozwa na sehemu kuu tatu katika maisha yake na sehemu moja ikiwa na matatizo maisha yake yote yanaweza kuharibika.  Sehemu hizi tatu lazima uzingatie ukuaji wake kila sehemu kutokana na mahitaji yake ya ukuaji.  Mara nyingi hua tunakoseaa tunakuza sehemu moja nyingine tunaacha hivyo inatuletea shida kwenye sehemu zilizobakia. 


Sehemu hizo tatu ni:  1. Mwili 2. Roho 3. Nafsi 
Sehemu hizi kuu tatu ndizo zinabeba maisha ya Mwanadamu na ukiona mtu anafanya mambo yasiyoeleweka  utakuta kuna sehemu haijafanyiwa kazi vizuri. 

1. Mwili
Wengi wetu hua tuna pambana zaidi na mwili kwa kuulisha kwenda hospitali kutibiwa n.k tunasahau zile sehemu nyingine. Mwili wako unahitaji afya bora ili uweze kufikiri vizuri, uweze kufanya uzalishaji bora, uweze kumuabudu Mungu wako. Kama wewe ni mgonjwa na umelala kitandani kuna mambo mengi utashindwa kufanya kwenye dunia hii. Hakikisha mwili unapata chakula bora,  fanya mazoezi kila siku. Huu mwili ndio kila kitu akili ikifikiria peke yake bila mwili kufanyia kazi zile fikra  hazina maana. Mwili ukiwa mbovu karibia kila sehemu itasumbua. Hakikisha mwili wako unakua na afya bora. 

2.Roho.
Roho yako nayo pia inahusika kwa kiwango kikubwa katika kupata matokeo bora ya vitu unavyovifanya.  Kutokana na imani ike unayoiamini  ndio inahusika katika kukuza Roho yako. Ukiwa na matatizo ya kiroho huwezi kufanya vyema kwa upande wa mwili utafanya kazi kwa bidii sana lakini kama roho yako ina matatizo utajikuta unakwama. Mambo yatakua hayaendi. Hakikisha unafuatilia vizuri imani yako ili ihusike katika ukuaji wa Roho yako. 


3. Nafsi. 
Hapa ndipo panakuaga na matatizo makubwa zaidi. Ukiweza kutengeneza mahusiano Mazuri na Mungu, ukala vizuri ukafanya mazoezi vizuri. Ukasahau nafsi yako utajikuta huendelei vyema. Nafsi ni wewe wa ndani wewe unaefikiri na unae amua kufanya vitu mbalimbali, unaemua kula, unaeamua kufanya mazoezi, unaemua kwenda kumuabudu Mungu wako. Ukuaji wa nafsi unatokana na kile unacholisha akili yako kila siku. Ili wewe ukue sasa na ufanye maamuzi yenye manufaa makubwa. Unahitaji kukuza akili yako vya kutosha. Unahitaji kusoma vitabu vya maendeleo binafsi sikiliza videos na audio za kufundisha.  Wengi wetu tuliacha kukuza akili zetu pale tu tulipotoka shuleni.  Ukiachana na shule kuna vitu vingi na vya muhimu sana vya kusoma ili uweze kua na matokeo bora duniani, ili uweze kua na ufanisi wa hali ya juu lazima usome vitabu. Mimj nakwambia soma vitabu kila siku angalau kurasa kadhaa tumia nusu saa kila siku kukuza ubongo  wako. Utakua na matokeo bora. 

Ili uweze kufanya vyote kwa pamoja unaweza kujijengea tabia ya kuamka saa kumi na moja alfajiri ukatenga muda wa: 
 1. Kujiunganisha  wewe na imani yako, 
 2. Soma vitabu 
 3. Fanya mazoezi. 

Ukiweza kufanya hivi kila siku na utajijengea maisha yenye matokeo makubwa na yenye furaha wakati wote. 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading