Connect with us

Ukweli ni huu Usijidanganye.

USIISHIE NJIANI

Ukweli ni huu Usijidanganye.

Zichukulie pande zote ni sawa. Wakati mwingine hua tunajidanganya wenyewe kwa kukataa kuambiwa ukweli. Umeanza biashara unataka kila unaemueleza akwambie nenda kafanye ni wazo zuri sana utafanikiwa akija mwingine akakueleza changamoto utakazokutana nazo unamwona mtu yule ni mbaya na hafai. Ukweli ni kwamba kwenye chochote kizuri na chenye matokeo mazuri changamoto ni lazima huwezi kuzikwepa […]

Zichukulie pande zote ni sawa.
Wakati mwingine hua tunajidanganya wenyewe kwa kukataa kuambiwa ukweli. Umeanza biashara unataka kila unaemueleza akwambie nenda kafanye ni wazo zuri sana utafanikiwa akija mwingine akakueleza changamoto utakazokutana nazo unamwona mtu yule ni mbaya na hafai. Ukweli ni kwamba kwenye chochote kizuri na chenye matokeo mazuri changamoto ni lazima huwezi kuzikwepa ni lazima uzipitie ili ufikie yale mazuri. 
Hivyo yote utakayoambiwa kuhusu kile unachokifanya yachukulie ni sawa  isipokua tu wale wanaokwambia huwezi,  utashindwa,   achana na hiyo biashara,  hao achana nao kabisa na usiwasikilize lakini ukikutana na mtu akakwambia biashara unayokwenda kuianza utakutana na changamoto hizi na hizi mtu huyu anakueleza ukweli.  Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kua hatuwezi kuyakwepa matatizo yetu kwa kujidanganya kua hayapo. Na wewe pia usijidanganye kwamba hakuna changamoto kwenye hicho unachokifanya ni kuzielewa na kupambana nazo.

Asante sana na Karibu

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in USIISHIE NJIANI

To Top