Zichukulie pande zote ni sawa.
Wakati mwingine hua tunajidanganya wenyewe kwa kukataa kuambiwa ukweli. Umeanza biashara unataka kila unaemueleza akwambie nenda kafanye ni wazo zuri sana utafanikiwa akija mwingine akakueleza changamoto utakazokutana nazo unamwona mtu yule ni mbaya na hafai. Ukweli ni kwamba kwenye chochote kizuri na chenye matokeo mazuri changamoto ni lazima huwezi kuzikwepa ni lazima uzipitie ili ufikie yale mazuri. 
Hivyo yote utakayoambiwa kuhusu kile unachokifanya yachukulie ni sawa  isipokua tu wale wanaokwambia huwezi,  utashindwa,   achana na hiyo biashara,  hao achana nao kabisa na usiwasikilize lakini ukikutana na mtu akakwambia biashara unayokwenda kuianza utakutana na changamoto hizi na hizi mtu huyu anakueleza ukweli.  Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kua hatuwezi kuyakwepa matatizo yetu kwa kujidanganya kua hayapo. Na wewe pia usijidanganye kwamba hakuna changamoto kwenye hicho unachokifanya ni kuzielewa na kupambana nazo.

Asante sana na Karibu

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading