461; Kanuni 3 za Mafanikio Makubwa

jacobmushi
2 Min Read

Zipo Kanuni tatu ambazo ukiweza kuzifanyia kazi maisha yako lazima yawe na Mafanikio.
Kanuni hizo ni:

1.Anza na Ulichonacho.

Usiwe mmoja wa wale watu wanaolalamika hawana mtaji, hawana msaada fulani wamekosa hiki na kile. Angalia kile ulichonacho na kitumie kuanza chochote kitakachoweza kukuingizia kipato. Jitazame na ufanye tathmini ya vitu ambavyo unavyo kuanzia ndani yako hadi nje. Angalia unajua nini, unamiliki vitu gani hapo unapoishi na unaweza kuvitumiaje vikuingizie kipato.


2. Fanya kile Unachoweza.

Usiwe mmoja wa wale watu ambao wanapendelea sana Kujitetea na kutoa sababu nyingi kwanini hawawezi. Angalia kile unachoweza ufanye. Unaweza kuongea vizuri na watu Hongera tumia hiyo kama njia ya kupata wateja.Unaweza kutengeneza bidhaa fulani tengeneza. Unaweza kuandika andika, una uzoefu fulani utumie. Usikubali kusema huna Unachoweza hakuna mwanadamu asiwe na kitu anachoweza kufanya labda wagonjwa mahospitalini.Unapofanya Unachoweza unaendelea kupata nafasi ya kujifunza mengine mengi zaidi.


3. Wekeza Kile Kile Kidogo unachopata.

Ndio usiwe mmoja wa wale watu ambao wakipata elfu kumi wanaitumia yote bila ya kuweka akiba hata ya tsh elfu moja.Umepata elfu kumi toa elfu moja itunze kisha ndio uanze kutumia ile elfu tisa.Hii elfu moja baada ya miaka michache haitakuwa elfu moja zitakuwa elfu nyingi.Kama hujui pa kuwekeza jifunze nione hata mimi nitakuelekeza.Usiwe yule mtu anasema kipato changu ni kidogo hakitoshi kuweka akiba, lakini wakati huo huo analipa kodi kwa kipato kile kile kidogo. Kama serikali inakukata bila kujali una elfu moja au laki kwanini wewe usijiwekezee asilimia kumi? 


Usikubali kuwa mtu wa matumizi makubwa kuliko unachokipata. Watu ambao unataka wakuone una maisha mazuri hawana msaada wowote na wewe.
Kuna Wakati nimekaa nikawaza nikaja kugundua kumbe wale watu niliokuwa nawahofia sana watanionaje ndio watu ambao hata vitabu nilivyoandika hawajawahi kununua hata kimoja. Kumbe tunaowahofu hawajali chochote kuhusu wewe.


Huu ni mwezi mpya jitahidi upige hatua. Jitahidi uongeze kitu kwenye maisha yako. 

Rafiki Yako

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading