UMEFANYA NINI LEO KUTIMIZA ILE NDOTO?

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Kila mmoja wetu ana ndoto  na maono ndani yake, hata mtu ambaye ni fukara kabisa ana ndoto ya kutoka kwenye  umaskini siku  moja.  Ukubwa wa ndoto zetu unatofautiana kila mmoja anaona kutokana na mazingira na taarifa alizonazo.

♻️Nataka ujiulize swali moja leo. Unafanya nini kila siku ili kufikia hiyo ndoto yako?  Unaendelea na maisha yako ya kawaida kila siku au kuna chochote kipya umejifunza au umefanya?

♻️ Wanadamu tuna tabia moja ya kipekee na inaturudisha nyuma sana. Mtu atafanya kazi kwa bidii sana pale anapopita kwenye magumu. Unatakiwa ujijengee tabia ya kufanya jambo iwe ni wakati unapenda au hupendi.

♻️Leo umefanya nini kipya?  Umejifunza kitu gani kipya?  Bila hivyo ujue tu kwamba kusogea itakua ni ngumu. Haiwezekani ukafika kule unakotaka kama hupigi hatua yeyote.  Hutaweza kubadili chochote kama ufahamu wako uko pale pale.

♻️Hutaweza kukua kama  huli!  Kama huilishi akili yako hutaweza kukua. Kama huilishi roho yako huwezi  kukua kiroho. Wewe kila siku  unajaza uchafu kwenye  akili yako. Habari zisizo na maana ndio unazifahamu kuliko mafundisho. Huwezi kukua.
♻️Kile kimjazacho mtu ndicho kimtokacho.  Kama wewe asubuhi utakula kiporo au chakula kilichochacha unategemea baadae itakuaje!? ? Lazima utawasumbua watu kwa harufu mbaya. Hivyo hivyo na ufahamu wako ukiujaza vitu visivyofaa asubuhi asubuhi  unatengeneza afya ya aina gani?

♻️Wewe upo tayari kusambaza habari  za kutisha tisha tu kwenye  magroup kuliko Makala kama hii hapa. Tena ukiona  imeandikwa unasema ndefu sana. ? Hivi mbona hua unajaza chakula tumboni hausemagi ni kingi sana?

♻️ Kama ulikua hujui  ni kwamba ufahamu wako ndio utakuwezesha kufika kwenye ndoto na maono yako.  Hivyo basi anza kubadili kile unachokiweka ndani ya ufahamu haraka sana.
“If you want to change the outputs change first the input ” ukitaka  kubadili changamoto nyingi unazopitia anza kubadili unachoweka akilini mwako.  Kuna matatizo mengine unapitia sio kwa sababu ni changamoto za kawaida ila ni kwa kua akili haina kitu.

♻️Matatizo hayawezi kutatuliwa kwa ufahamu ule ule uliyoyatengeneza. Ili uweze kubadili matatizo uliyonayo kuza ufahamu wako. Unakuza ufahamu  kwa kusoma, kusikiliza, na kuona. Tafuta maarifa kila sehemu utayapata. Sikiliza audio books. Utaweza kufika kule unapotaka.

♻️ Ukidhamiria Unaweza kuamua siku isipite bila kuongeza kitu kipya kwenye  ufahamu wako. Na hiyo ndio hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye  mafanikio makubwa zaidi.

UMEFANYA NINI LEO KUTIMIZA ILE NDOTO Yako? Unakwenda kufanya nini leo?
 Karibu sana
Jacob Mushi
Phone 065472668
Email jacob@jacobmushi.com

Jipatie vitabu hapa… http://mushijacob.blogspot.com/p/vitabu-vya-sauti?m=1

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading