Ukweli ni kwamba hakuna mtu asiyependa mafanikio, hata maskini kabisa anatamani sana atoke kwenye umaskini wake awe na mafanikio. Tatizo linakuja kwenye kile ambacho mtu anakifanya ili awe na mafanikio. Sasa cha ajabu ni kwamba watu wanafanya vitu kila siku lakini hawajui kama wanavyovifanya ni sahihi au lah.

Leo nataka ujiulize swali hili la muhimu “ni wapi Nakosea?” kwanini sipati matokeo ninayoyataka? Kwanini ninachukua hatua lakini nabakia pale pale siku zote? Jibu ambalo nataka kukupa ni kwamba unafanya vitu vingi sana lakini sio vitu sahihi katika vile ambavyo vinaleta mafanikio.

Watu wengi wanaamka asubuhi na mapema lakini kinachowafanya waamke mapema ndio kinatofautisha katika matokeo ya siku ya mtu. Kuna mtu ataamka mapema ili awaandae Watoto wawahi shule. Mwingine ataamka mapema ili awahi kazini, mwingine ataamka mapema kwasababu tu kuna foleni njiani hivyo anaamka ili awahi foleni.

Kitu kimoja ambacho wengi wanasahau sio kile kinachokufanya uamke mapema ndio kinaleta mafanikio yako ya siku. Kinacholeta mafanikio ya siku yako ni kile unachokifanya baada ya kuamka. Wewe unafanya nini unapoamka?

Robina Sharma Mwandishi wa kitabu kiitwacho The Leader Who Had No Title, yaani kiongozi asie na cheo, pia ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana katika mambo ya uongozi, amekuwa akinifundisha kwa muda mrefu vitu ambavyo unatakiwa kuvifanya kila siku ukiamka asubuhi. Mambo haya na wewe unapaswa kuyajua Rafiki yangu ili uweze kuwa na siku yenye mafanikio makubwa.

Unapoweza kuwa na siku yenye mafanikio makubwa utatengeneza wiki yenye mafanikio makubwa. Unapoweza kuwa na wiki yenye mafanikio makubwa basi  unatengeneza mwezi wa mafanikio makubwa na hivyo inakuletea mwaka na miaka yenye mafanikio makubwa.

Rafiki yangu mimi nataka kukwambia kuwa unapaswa kubadili kile unachokifanya kama unataka matokeo makubwa. Badala ya kuamka na kuanza kufanya yale ambayo umezoea kufanya siku zote mimi nitakuelekeza kitu cha kufanya kila unapoamka kwa dakika 20 tu na Maisha yako yatakwenda kubadilika kabisa.

Unawezaje sasa kufanya vitu hivi? miezi 3 iliyopita nimekuwa naendesha Program kwenye Mtandao iitwayo DAKIKA 20 ZA MAFANIKIO. Program hii ilikuwa ni kuwalekeza watu vitu vya kufanya kila wanapoamka asubuhi Programu hii imeleta matokeo makubwa kwa baadhi ya waliohudhuria.

Unawezaje kufahamu vitu hivi vya kufanya asubuhi? Ipo njia moja na ya pekee nayo ni kujiunga na Mafunzo ninayotoa kila mwezi ya Coaching. Unaweza kuyapata Hapa…. https://jacobmushi.com/kocha

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

One Response

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading