Kabla hujaanza kusoma Makala hii naomba ujiulize swali hili, yale mambo ulikuwa unasemaga nitafanya kesho umeshayafanyaga hata japo nusu yake? Najua jibu la wengi ni hapana. Hata Makala hii kuna wengi walisema watasoma baadae na hawatasoma tena. Rafiki yangu mafanikio huwezi kuyapata bila ya Nidhamu. Nidhamu ni kufanya jambo ambalo unatakiwa kulifanya kwa wakati unaotakiwa kulifanya hata kama hujisikii kulifanya kwa wakati huo. Sasa jiulize wewe una Nidhamu? Kitendo tu cha kusema nitafanya kesho hakuna mahali popote ulipo weka note kwamba hilo jambo utalifanya kesho ni tayari umeshalipoteza.

Chochote kinachoendelea kwenye Maisha yako sasa hivi, ni wewe umekitengeneza au umekiruhusu kitokee. Haijalishi ni ugonjwa, matatizo kwenye mahusiano yako, kazini unapofanya kazi, au chochote kizuri au kibaya kinachoendelea ni wewe umekitengeneza au umekiruhusu kiwepo kwenye Maisha yako.

Umetengeneza vipi?

Matokeo mazuri yeyote yanaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya kutosha kwenye kila jambo unaloamua kulifanya. Matokeo mabovu yanaletwa na kuahirisha mambo, uvivu, kulalamika, kutafuta wa kumlaumu, kutoa sababu za kutosha kwanini hujaweza au hujafanya jambo Fulani.

Umeitengeneza afya mbovu uliyonayo kwa kula vyakula visivyofaa huku ukijua kabisa. Umeharibu mahusiano yako kwa kuendekeza tabia mbovu ambazo hata wewe mwenyewe usingependa kufanyiwa. Una matatizo ya kifedha kwasababu ukipata pesa unatumia zote zikiisha ndipo unakumbuka kuweka akiba.

Yapo mengi umeyatengeneza na unaendelea kutengeneza kila siku. Hii ni kwasababu umeshajitengenezea mfumo mbovu wa Maisha yako. na huo mfumo ndio unaufuata kila siku kisha unakuletea matokeo unayopata.

Umeruhusu Vipi?

Kwa kushindwa kusema hapana kwa mambo ambayo hayafai ndio maana umeingia kwenye hali uliyonayo sasa. Kwa kujipeleka kwenye mazingira ambayo ni hatarishi bila ya kujali usalama wako ndio maana umeibiwa.

Umetembea kwenye njia ambayo unajua ina vibaka, huku umebeba vitu vya thamani, ukiibiwa

Umeruhusu watu waamue wewe uvae nguo gani, uende wapi kula, utumie usafiri wa aina gani na ndio maana Maisha yako yanazidi kuwa magumu wakati unapokea mshahara mzuri tu. Maisha yako yamekuwa magumu Zaidi kwasababu pesa unayoingiza ni nyingi lakini inaishia kwenye matumizi.

Soma: Tafuta sababu ya Tatizo

Umeruhusu watu wakuamulie kila kitu kwenye Maisha yako ndio maana unaendelea kuumia. Umeruhusu hali ya wewe kuwa tegemezi sana kwa wengine hadi inafikia wakati unaumizwa.

Ufanyeje?

Chukua maamuzi mapya ya kutengeneza na kuruhusu vitu ambavyo vina matokeo chanya kwenye Maisha yako. kabla hujafanya maamuzi yeyote kila wakati jaribu kufikiria mbele kwenye Maisha yako ya baadae. Yatazame maono yako na ndoto zako kubwa. Angalia maamuzi unayofanya leo yataleta matokeo gani kwenye Maisha yako miaka mitano ijayo?

Kama utafanya maamuzi mabaya basi utatengeneza na kuruhusu hali mbaya Zaidi ya uliyonayo sasa hivi.

Kila wakati unapotaka kufanya jambo ambalo unajua lina matokeo kwenye Maisha yako hakikisha umeangalia kule unakoelekea. Embu tazama hilo jambo linaleta mchango wa aina gani?

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading