Una uwezo mkubwa sana ndani yako, haijalishi upo kwenye haali gani sasa hivi.
Una uwezo wa kufanya mambo makubwa sana, haijalishi huna nini sasa hivi.
Una nguvu kubwa ya kuibadili dunia, haijalishi watu hawakuelewi kwenye kile unachowaambia.
Una nafasi ya kuacha historia mpya, haijalishi umefanya nini, umekosea wapi.
Leo ndio siku yako ya kipekee jana huna kazi nayo tena, kama ulifanya vizuri jipongeze na endelea mbele.
Elewa kwamba hakuna utakachokifanya upate matokeo kama yale uliyoyatarajia vikwazo vipo kila mahali na hiyo ndio asili ya dunia.
Milima na mabonde ni kwa ajili ya kukukomaza wewe ufikie sehemu uweze kusimama imara.
Kama umechagua kuwa mtu wa tofauti katika jamii inayokuzunguka usitegemee kupendwa usitegemee kusifiwa.
Kukataliwa ndio mwanzo wa wewe kupata kile unachokitaka, kupoteza marafiki na watu uliodhani watakua upande wako ndio mwelekeo wa kule unapopapigania.
Kamwe usiweke tegemeo lako kwa mtu maana, kuna wakati utakua unamhitaji sana na atakuvunja moyo na hutaamini.
Tumia kila rasilimali uliyonayo ili uweze kufikia kile unachokitaka kwenye dunia hii vyote vilivyopo duniani ni kwa ajili yetu ni kila mmoja kujua ni nini anataka na kuanza safari ya kukifikia.
Wanasema mvumilivu hula mbivu bila kuvumilia changamoto na vikwazo vyote unavyopitia hizo mbivu huwezi kuzila.
Haraka haraka haina Baraka, ni kweli ukifanya haraka hutafanya vizuri kwanza utachoka haraka kabla hujafikia kile unachokitaka.
Kile ulichoamua kukipigania kipiganie hadi mwisho, usikatishwe tamaa na watu hawajakiona kile ulichokiona wewe.
Kua mwaminifu kwako na kwa wengine, kile usichopenda kufanyiwa na wengine usiwafanyie wengine.
kama unachokifanya kinawasababisha wengine wawe na maisha magumu ujue hakifai maana hawawezi kukupa unachokitaka.
Kama ni pesa zipo mikononi mwa watu hivyo unachokifanya hakikisha kinawapa furaha wengine kinawarahisishia maisha wengine watakua tayari kukupa chochote unachokitaka.
Najua safari umeshainza kumbuka mambo yanapokua magumu usibadili malengo wala ndoto badili mpango.
Ili uweze kupata nguvu mpya kila siku na hasa pale unapokua kwenye wakati mgumu penda kujichanganya na watu wenye mtazamo kama wako wenye malengo na ndoto kubwa kama zako hao watakufanya wewe uendelee kupata nguvu Zaidi na kusonga mbele.
Nikutakie jumapili yenye Baraka tele.
Asante sana.
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668/0755192418 Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading