Kila mmoja ana kitu cha kipekee sana ndani yake ambacho amezaliwa nacho. Ni muhimu sana kutambua zawadi uliyozaliwa nayo ili uweze kuitumia kuyafanya maisha ya wengine kua mazuri. Kupitia unachokifanya kuna mtu anaguswa sehemu. Kwa kupitia unachokifanya kuna maisha ya mtu yanabadilika. Haijalishi ni kidogo kiasi gani lakini kuna mtu anafurahia kazi yako. Jiangalie hapo ulipo kuna vitu vingapi unavitumia ambavyo ni kazi za wanadamu wenzako? Ni vingi sana hata kifaa unachotumia kusomea hiki kitabu humjui alietengeneza lakini amefanya maisha yako kua bora. Sasa wewe ni kitu gani unafanya kinafanya maisha ya wengine kuendelea kua bora? Unayagusaje maisha ya wengine? Tumia zawadi Mungu aliyoweka ndani yako. Zawadi hii yaweza kua kipaji chako, ubunifu wako, kusudi lako, elimu yako, pesa zako, na vingine vingi, vitumie kuyagusa maisha ya wengine.

Usikubali kabisa uondoke duniani na hujatumia zawadi ulizokuja nazo.zawadi hizo zipo kwa ajili ya kuwafaidisha wengine ndio maana tupo wanadamu wengi tunaishi pamoja. Nimeamka asubuhi ya leo nikajitazama mimi na vyote vilivyonizunguka nikashindwa kuhesabu nimejikuta nina vitu karibu 100 tofauti tofauti ambavyo vimetengenezwa na wanadamu wenzangu. Wengine bado wapo hai wengine walishakufa. Na wengine siwajui kabisa nikasema na mimi kuna vingapi vyangu wenzangu wanafurahia. Hata wewe unacho cha pekee ndani yako unaweza kukitumia na kuongeza thamani kwa watu.

Tukizungumzia sifa za wanyama tunazungumzia kundi zima la wanyama mfano tukisema simba ana nguvu sana ni simba wote porini. Sijawahi kusikia jina la Simba mmoja ambaye ana kitu cha pekee tofauti na simba wengine sifa zao ni zile zile lakini wewe ni mmoja kati ya wanadamu bilioni 7 una sifa yako ya kipekee na una jina lako la kipekee, unafikiri kwa namna ya kipekee, unatembea kwa namna ya kipekee, Wewe ni Zaidi ya Simba, Zaidi ya Tai, Zaidi ya mnyama yeyote uliewahi kusikia sifa zake. Tukizungumza sifa za Tai hatuzungumzii tai mmoja tunazungumzia kundi lote la Tai lakini wewe ni wa kipekee sana hatuwezi hata kukuchanganya na wanadamu wengine tukasema unafanana nao. Ni kwanini? Kwasababu una zawadi ya kipekee sana ndani yako.

Itambue zawadi, itumie zawadi, yafanye maisha ya wengine kua bora na kwa kufanya hivyo maisha yako yanakwenda kua bora Zaidi.

Karibu sana
Jacob Mushi
0654726668
jacob@jacobmushi.com


Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading