Mwandishi mmoja wa vitabu anaejulikana kwa jina la Zig Ziglar Alisema “To get what you want you must help enough people to get what they want”  yaani kupata chochote unachotaka unahitaji kuwasaidia watu kupata vile wanavyotaka. Akiwa na maana kwamba kile unachokifanya kiwe kinagusa maisha ya wengine. Kama biashara unayoifanya haigusi maisha ya watu wengine kwa namna moja au nyingine uko kwenye biashara ambayo haitakupatia mafanikio.

Kwa kugusa maisha ya wengine ndipo na wao wanapotoa pesa zao ili tuendelee kuwagusa. Kama unachokifanya kinaleta furaha kwenye maisha ya wengine hawataacha kutoa pesa zao mfukoni kukupatia ili uwape huduma au bidhaa.

Hivyo basi tukubaliane kwba unahitaji watu wengi sana ili ufanikiwe. Watu wa aina mbali mbali na hapa ni hadi wale unaowaona wana mtazamo hasi kuna wakati watahitaji huduma yako au bidhaa yako hata kama walikukatisha tamaa.

Chochote kile unachokifanya kwenye dunia hii ili ufikie mafanikio makubwa unahitaji watu wengi zaidi. Kwa kifupi kama ni biashara basi Ukiweza kuwahudumia angalau watu milion moja utakua umefika mbali sana.

Jiulize leo ninachokifanya kinagusa vipi maisha ya wengine. Ukishafahamu vizuri ongeza juhudi na hakikisha unakua na ubora wa hali ya juu.

Weka malengo ya kila baada ya muda fulani unataka uwafikie watu wangapi na fanyia kazi malengo yako hata yatimie.

Hata kama unazibua vyoo ili ufanikiwe unahitaji uzibue vyoo vya watu wengi zaidi. Na hao watu utazibuaje vyoo vyao kama huna mahusiano bora nao?

Ninakubali kwamba huwezi kua rafiki wa kila mtu lakini haina maana kwamba ambao sio marafiki zako ni maadui zako. Jifunze kuishi na kila mtu kwa vyovyote vile alivyo kwa kua kuna vitu unaweza kufaidi kwake.

Unahitaji watu ili uweze kufanikiwa na kadiri ulivyo na ndoto na malengo makubwa ndivyo idadi ya watu unaowahitaji inakua kubwa.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Mwandishi  Kocha wa Mafanikio na Mjasiriamali.

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading