Mafanikio hayamtaki mtu mvivu, mtu mzembe, anaeahirisha mambo, anaetazama Zaidi kule alipotoka kuliko anapokwenda. Mafanikio yanamtaka mtu ambaye ameamua kutoka moyoni mwake kuwa anayataka mafanikio.

Usikubali kabisa kuingia kwenye mtego wa kuchanganya mambo, kama umeamua kuwa muumini wa mafanikio amua kweli na uzifuate kanuni na misingi. Ukiwa mtu wa kuchanganya mambo, leo unataka hiki kesho umeenda huku utapotea.
Utakuwa unajisogeza kwenye shimo kama bado utakuwa unatamani tabia zilizokuwa zinakufunga usione mbele.

Unajisogeza kwenye shimo kama bado kuna aina ya Maisha ambayo ulishaishi unataka yajirudie, maana yake wewe unataka kurudi ulipotoka.

Kama umeamua kuwa tai lazima ukubali kufuata tabia za tai. Ukichanganya utakuwa kiumbe asie eleweka.

Usikubali kujitegea mtego mwenyewe kwa kuyatamani mambo yaliyopita kwani hakuna namna ya kurudi ulipotoka.

Usikubali hata kidogo ulikotoka kukafanyika sababu ya wewe kutokusonga mbele.
Kama husongi mbele ndugu yangu unarudi nyuma. Endelea kuangalia unapokwenda usikubali chochote kikufanye upoteze muelekeo wa safari yako ya mafanikio.

Uhai wako una maana sana hapa duniani, haujabaki hai kwa bahati mbaya. Endelea kusonga mbele Mungu ana kusudi na wewe.

Tamani Kusonga mbele Kila wakati, bila kujalisha upo kwenye nyakati zipi.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading