“UNAJUA KWANINI UMESHINDWA”
Habari ya leo msomaji wetu. Tunashukuru kwa kuendelea kututia moyo kwa kusoma pamoja nasi. Ubarikiwe sana. Leo tuna jifunza “unajua kwanini umeshindwa?”
Unajua kwa nini biashara ulioianza ulishindwa? Kwanini kipaji chako umeshindwa kukiendeleza? Kwanini ulitamani sana kufanya jambo fulani zuri lakini limeshindikana?
Kwanza kabisa kama hujalifanya hilo jambo unalozani umeshindwa basi ujue hujashindwa “huwezi kusema umeshindwa kitu fulani kabla hujakifanya” ili ufeli au ufaulu mtihani lazima uingie kwenye chumba cha mtihani. Usipofanya mtihani matokeo yako utawekea desh. Sasa wewe kabla hujasema ujasema umeshindwa hakikisha kwanza umefanya.
Kama umefanya ni sababu ipi hasa iliyokufanya ushindwe? Mimi nakutia moyo kua usichoke kurudia tena na tena kwani hata Shetani alipomjaribu mara 3 Yesu akamwambia nenda zako shetani. Ingewezekana kama asingeambiwa aende zake angeendelea kumjaribu. Usikate tamaa kwa lile unalodhani umeshindwa endelea kujifunza. Kushindwa kwako kuwe changamoto ya kujifunza. Lile eneo unaloliona ni gumu nenda kajifunze zaidi ili uweze kulivuka.
Katika safari yetu ya maisha hapa duniani watu waliofanikiwa wote walipitia mambo mengi magumu sana ule ugumu waliopitia ndio unawafanya wanadumu mpaka sasa. Usiogope magumu unayopitia yanakujenga uwe mtu bora hapo baadae. Yesu angeogopa kufa msalabani sidhani kama tungekua tunamfahamu leo hii kama Mkombozi wa ulimwengu. Mateso aliyopitia ndio thamani ya yeye kua Mkombozi wetu. Pia wewe magumu unayopitia ndio yanayokutengeneza ili uwe imara.
Katika moyo wa mwanadamu mara nyingi kuna sauti mbili sauti ya nafsi yako(moyo) na akili yako. Hivi hua ndio vinazungumza wakati unapotaka kufanya jambo. Moja itakwambia huwezi nyingine itakwambia unaweza. Matokeo huja pale unapochanganya na ushauri wa marafiki na ndugu. Endapo sasa hao marafiki na ndugu wakiwa upande wa kukwambia huwezi na wewe ukakubaliana nao utashindwa tu.
Mimi leo ninakwambia hakuna linaloshindikana katika dunia hii. Inahitajika nia inayotoka ndani yako. Una uwezo mkubwa sana tu jifunze kuutumia utaona mambo yanaenda sawa.
Asante sana kwa kusoma makala hii ni matumaini yangu umejifunza. Imeandikwa na Steven Mshiu . 0655882074
Karibu sana.
Karibu sana.