Unakwenda Wapi?

jacobmushi
2 Min Read
Mwaka 2016 Inawezekana umekuonyesha picha ya unapokwenda au umekufanya ukapoteza kabisa mwelekeo wako.

Leo Rafiki nataka ujiulize hili swali, Unakwenda wapi?  Embu tafakari ulipotoka miaka yote hadi ulipo sasa!  Unaelekea wapi?  Je unafikia ndoto yako au unapotea?

Najua kabisa na ninaelewa kwamba yako Mambo mengi unapitia ya maisha. Mengine ni Magumu sana yanaumiza moyo. Lakini ni muhimu sana kukaa chini na kujiuliza unakoelekea. Kama unaelekea shimoni ni wakati wa kusimama na kutafuta Njia sahihi.

Wengi tumekuwa tunafanya mambo mengi  sana ili kujipatia pesa pekee. Lakini tumesahau mambo ya msingi sana. Ndio maana wengi huchoka kabisa na kusema pesa hazikuletei furaha.

Unajua ni kwanini watu wanafikia kusema hayo?  Kwasababu wamekua watumwa wa pesa, wanatafuta pesa hadi wanaishia kuwa watumwa. Pesa zinaingia mifukoni kisha zinatoka inabidi wakatafute tena.

Hata kama biashara zako zinakutengenezea pesa nyingi kiasi gani kama unachokifanya hakiendani na kilichokuleta duniani huwezi kuwa na furaha hata siku moja. Utaishi kwa hofu, mashaka,  na mwisho utakuja kupoteza kila kitu.

Kaa chini Kabla mwaka huu haujapita na jiulize Unakwenda wapi? Duniani upo ili kufanya nini?  Kwani Ulizaliwa kuja kutafuta pesa?  Hapana!  Pesa walizitengeneza wanadamu!  Sikwambii usitafute pesa. Nakwambia lengo lako kuu la maisha lisiwe kutafuta pesa utakuwa mtumwa.

Embu jiulize upo duniani mpaka sasa, umeshafanya kitu gani kuacha alama. Dunia itasema kulikuwepo na mtu fulani hapa duniani karne ya 21 alifanyaga nini? Usikubali kabisa kuondoka ukiacha vitu vinavyoharibika baada tu ya wewe kuondoka.

Jiunge na Semina Ya MABADILIKO Ya KIFIKRA NA Kiuchumi uweze kugundua Mambo mengi sana na ya muhimu katika maisha.

Tuma ujumbe wenye neno Semina kwenda no 0654726668

Nimekuandalia Zawadi nzuri sana Kipindi hiki cha siku kuu tafadhali Bonyeza hapa kuchukua zawadi yako 

Karibu sana Rafiki Yangu.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
Email: ushauri@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com,  www.jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading