Kuna nyakati unaweza kukutana na fursa mbele yako kabisa halafu ukapishana nayo kama vile hukuiona kwasababu unajiona hustahili.

Kuna mambo makubwa yanaweza kujisogeza karibu yako kwasababu ni Mungu anayaleta na anajua wewe unastahili hayo ila kwasababu unajiona wewe ni mdogo sana, wewe ni dhaifu sana hivyo hata uwezo wa kuona fursa ile unakuwa haupo.

Inawezekana huendelei mbele sio kwasababu huna uwezo au hujajaribu vitu ila ni kwamba kuna vitu unaviogopa kuvifanya kwasababu tu akili yako na moyo wako unakwambia wewe hustahili kitu hiki, wewe vitu vyako ni vya saizi ile.

Ukianza kujitambua na kuona unastahili vikubwa ndipo utashangaa milango inafunguka na wewe unatoka hapo ulipo.

Ondoka kwenye vifungo vya kujiona hustahili kwani ndio vinakuzuia wewe usiweze kuifikia lile ambalo Mungu ameweka mbele yako.

Kuna watu unashindwa kukutana nao kwasababu unajiona hustahili, inawezekana mke au mume wako mtarajiwa yupo sehemu anakusubiri lakini unashindwa kumuona kwasababu unajiona hustahili. Napenda kukwambia wewe unstahili vitu vikubwa.

Anza sasa kujitengeneza kuanzia ndani akili yako, na moyo wako uanze kuona na kuamini kwamba unastahili vikubwa, achana na nje yako, achana na yale ambayo unayaona ni madogo umeyafanya. Wewe unastahili vikubwa endelea mbele chukua fursa kubwa zinazokuja mbele yako.

Kamwe usikubali kujiambia kwamba wewe hustahili hiki au kile, hustahili kuwa na mtu Fulani kwasababu ni mtu mkubwa sana, hapana kama ni kusudi Mungu lazima litimie ila unaweza kulichelewesha kwa kujiona hustahili.

Shetani ni mbaya sana anaweza kukuletea vitu ambavyo sio vyako na wewe ukajikuta unavipokea halafu baadae unakuja kugundua kile chako ulipishana nacho. Kwa wewe kuingia kwenye mtego wa shetani unakuta ndio unaziba ule uwezo wa kupata kile chako halisi, kuwa makini usije kuingia kwenye mtego.

Hakikisha kila siku unapoamka unajisemesha kwamba unastahili mambo makubwa, unastahili vitu vikubwa kwasababu wewe ni mtu mkuu sana. Mimi naamini hivyo juu yako anza na wewe kuamini ili itokee bila Imani hakuna kinachowezekana hata kumpendeza Mungu haiwezekani.,

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

2 Responses

  1. am so thankful to u’re doctrine manservant be blessed a lot, but sory am asking for book related with success may I receive it by which means?

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading