#USIISHIE_NJIANI- UNASUKUMWA NA NINI KUFANYA UNACHOKIFANYA?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Habari rafiki, siku yako umeianzaje? Hakikisha unasali, unasoma kitabu, unapitia maono na malengo  yako na unafanya mazoezi. Hii itakufanya uwe na siku bora yenye uzalishaji.

Mtu mmoja akaniuliza kwamba “ tunatafuta pesa za nini kama tutaondoka na kuziacha zote?”

Akanieleza hadithi ya rafiki yake aliekuwa mpambanaji kweli ikafikia kipindi pesa ndio zilikuwa zimeanza kuingia mikononi mwake. Lakini ghafla akaondoka duniani huku amecha mke mzuri sana na watoto.

Rafiki yule akasema hivi tunavyovitafuta ni vya kazi gani kwanini mtu asitafute hela yake ndogo ya kumwezesha kula na kuishi kila siku tu?

 

Nilichojifunza kwamba watu wengi hawajui maana ya Maisha. Hatuishi hapa duniani kwa ajili yetu. Hatutafuti pesa kwa ajili yetu tufanya kwa ajili ya wengine.

Lolote unalofanya sasa hivi unaweza usilifaidi sana kama kizazi kijacho. Sisi wenyewe tunafurahia kazi nyingi za watu miaka iliyopita. Unachopaswa kufanya ni usikubali kuishi bila kutoa kile ambacho Mungu ameweka ndani yako.

 

Baraka zako zipo kwenye kile ambacho umezaliwa kuja kukifanya. Mafanikio yako yapo kwenye zawadi Mungu alioweka ndani yako. usifanye kazi kwasababu unataka pesa tu ndugu utapotea. Ipo siku hizo pesa utazipata lakini utakosa za kufanyia. Tafuta pesa huku unajua kwanini upo duniani na kuishi kusudi lako.

Ili kuepusha majuto ndani ya nafsi zetu ni sisi kuweza kuishi kile ambcho kimetufanya tuje hapa duniani.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

 

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading