Unawezaje kubadili hali uliyonayo sasa hivi?

jacobmushi
By jacobmushi
4 Min Read

Kabla hujaanza kubadili chochote lazima ufahamu chanzo cha hali uliyonayo kimesababishwa na  nini. Ukweli ni kwamba mfumo wako wa maisha unajengwa na mambo haya yafuatayo.

FIKRA
Kila kitu kinaanzia kwenye mawazo/fikra zetu kama unajiona upo kwenye hali mbaya sana kipindi ujue imesababishwa na mawazo uliyoyawaza kipindi Fulani. Kama kuna kitu cha muhimu cha kuchunga ni mawazo ni kile kitu unachokiwaza kila siku maana ndio vinatengeneza mfumo wako wa maisha, ndio vinaaamua uwe hivyo ulivyo leo.
Unawezaje kulinda mawazo yako?
Kwanza tunaanza na vitu unavyovisikiliza kila siku, kama wewe ni mfuatiliaji wa habari mbaya kila utakachokua unakiwaza kitakua ni kibaya hata story zako zitakua ni mbaya, unaangalia nini ni habari zinazokujenga au ni matukio yanayotokea kila siku, Unasoma nini unachokisoma kinaingia kwenye akili yako hivyo kitatengeneza mawazo ambayo utakua unayawaza kila siku. Angalia vitu hvyo vya muhimu ili uweze kulinda mawazo yako na utakua na matokeo bora

MANENO
Maneno yanaletwa na mawazo chochote unachokiongea ulikiingiza wewe mwenyewe kwenye akili yako kwa kupitia KUSIKILIZA, KUANGALI NA KUSOMA. Kama unataka kubadili maneno yako badili unachokisikiliza kila siku, unachokiangalia na unachokisoma, utabadili fikra zako na maneno yako yatabadilika. Haiwezekani mtu afuatilie  mpira kila siku halafu aongelee habari za siasa, vilevile haiwezekani mtu afuatilie habari za siasa halafu aje aongelee habari za mafanikio.

MATENDO
Mawazo yako na maneno yako yatakusababisha wewe uingie kwenye matendo ya kitu Fulani na siku zote matendo yana matokeo, kwa vyovyote vile unachokitenda sasa hivi kina matokeo makubwa ya sasa na ya baadae. Kama tunavyojua chochote kinachotokea sasa hivi kwenye maisha yako ni matokeo ya fikra zako na matendo uliyoyatenda huko nyuma kitu cha kwanza cha kubadili ni fikra zako
.
TABIA
Ukifanya jambo lolote kwa mfululizo hugeuka kua tabia yako kwa hiyo angalia una matendo ya aina gani, je una aihirisha mambo? Unasema utaanza kesho, na hujaanza hadi leo? Itakua tabia yako na utajikuta una aihirisha kwenye kila jambo. Badili fikra , manano yatabadilika, na vitendo vitabadilika na tabia itabadilika.

MFUMO WA MAISHA
Tabia inatengeneza mfumo wa maisha kwa mfano umejijengea tabia ya kuamka saa kumi na moja alfajiri huo ndio utakua mfumo wako wa maisha, labda uamue kuubadili,  umejijengea kila asubuhi lazima upitie magazeti, huo utakua ni mfumo wako wa maisha, umejijengea tabia ya kulalamika na kulaumu huo utakua mfumo wako wa maisha. Ukitaka kua na mfumo mzuri wa maisha anza kubadili tabia ndogo ndogo ulizonazo na tabia utaanza kuibadili kwenye chanzo ambacho ni fikra, kile unachokiingiza kichwani ndio cha kubadili.

HATMA
Mfumo wa maisha unatengeneza hatma yako, hatma ni mwisho wako utaishiaje, mfano wewe ni jambazi hatma yako inajulikana wazi kua utakuja kuuliwa, vile vile kwenye chochote kile kiwe kizuri au kibaya hatma yako unaweza kujua wewe mwenyewe, kama utakufa maskini angalia matendo yako, tabia zako na mfumo wako wa maisha ukoje hapo utajipatia jibu la hatma ya maisha yako huhitaji kwenda kwa Nabii, Mtabiri, Msoma Nyota wala Mganga wa kienyeji. Angalia tu matendo na tabia ulizo nazo kila siku.
Anza leo maisha yako yatabadilika ni kuchukua hatua tu kilichobakia na kuanza kufanya .

Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie jacob@jacobmushi.com No 0654726668

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading