Nakumbuka nimewahi kuandika mahali kwamba “Maisha yako Ni Tabia Zako” yaani vile unavyoishi kila siku ni mkusanyiko wa tabia ambazo umezitengeneza. Ni rahisi sana kutengeneza tabia mbaya kuliko tabia nzuri. Unajua ni kwanini? Mara nyingi tabia mbaya mwanzoni ni nzuri na ni rahisi, tabia nzuri mwanzoni ni ngumu na zinachosha.

Unapoanza kuamka mapema utaanza kuona kama ni mzigo Fulani mzito lakini ukishajenga hiyo tabia utaanza kuifurahia. Mimi kwa Zaidi ya miaka kumi sasa nimekuwa sili chakula cha mchana, na ikitokea nimekula basi jioni ninaweza kula matunda tu au kitu chepesi na nikalala bila shida yeyote. Mwanzoni watu walikuwa wanasema wewe utapata vidonda vya tumbo na mengine  mengi lakini hadi sasa sijawahi hata kuona dalili.

Nimekuwa nalala saa tisa au saa kumi kwa muda wa miezi sita iliyopita na ikitokea nimelala mapema basi nitakuwa nimechoka sana. Sasa kitu cha ajabu ni kwamba kumbe nimekuwa natengeneza tabia bila kujua. Nikilala masaa sita tu basi nitaamka mwenyewe bila hata ya kuamshwa na alamu. Nimejikuta kwamba nikilala saa nne kamili usiku saa tisa au saa kumi ninakuwa nipo macho na usingizi umekwisha kabisa.

 

Ili uweze kutengeneza tabia yeyote ambayo itakuja kukusaidia andika tabia hizo chini zote na zifanyie kazi kwa muda mrefu hadi ziingie kabisa kwenye mfumo wa akili zako. Kama ambavyo mtu anaweza kuwa mlevi na ikawa ngumu kuacha na wewe pia unaweza kutengeneza ulevi kwenye vitu ambavyo vinaweza kukusaidia.

Lazima ukubali kujipa muda wa kufanya hadi uone matokeo yanaanza kuja. Sio kitu cha siku moja ambacho umeamka leo kesho tayari. Ukiona unafanya vitu vyenye matokeo ya muda mfupi ujue vit hivyo havidumu kwa muda mrefu. Mfano ni mhindi unaweza kutoa mahindi baada ya miezi mitatu lakini ukitoa mahindi mara moja hauwezi kutoa tena. Lakini mwembe unaweza kukaa miaka mitano ndio ukaanza kutoa matunda na baada ya hapo itapita miaka na miaka ukitoa matunda tu. Tengeneza tabia ambazo utakuja kuzifaidi Maisha yako yote.

Ukiweza kutengeneza tabia nzuri ni kwa faida yako mwenyewe. Unakuwa na Maisha ambayo wewe mwenyewe unayafurahia. Unatengeneza aina ya Maisha ambayo yanakuwa bora Zaidi kwako na kwa wale wanaokuzunguka.

 

Usiishi Maisha ya kuiga wengine, kununua vitu kwasababu watu wananunua, kufanya mambo kwasababu umeona kila mtu anafanya. Unaweza kuchagua kuishi vile unavyotaka wewe kuishi. Ubora wa Maisha yako ni ubora wa tabia ambazo umeamua kuzitengeneza na kuziishi kila siku.

 

Chochote unachokifanya hata kiwe cha hovyo kiasi gani kina matokeo huko mbele unakoenda. Usikubali kufanya vitu ambavyo huvitaki vitakuja kukutesa. Yaani namaanisha usikubali kutengeneza tabia ambazo hutapenda kuja kuishi nazo huko baadae. Tabia ambazo zitakuwa ni aibu watu wengine wakijua unafanya. Usikubali kutengeneza tabia ambazo zitakuja kukutesa baadae.

Tabia Ambazo zinaweza kukufanya uwe bora:

Lala Mapema, amka Mapema.

Soma Vitabu.

Andika.

Pangilia Ratiba ya Siku, Wiki, Mwezi na Hata Mwaka. Kuna watu ambao ukitaka kuwaalika mahali unapaswa uwajulishe miaze sita kabla, la sivyo huwezi kuwapata.

Fanya Mazoezi.

Omba.

Nyingine Ongezea Mwenyewe.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading