“Kijana mmoja alichukua kisu akataka kujiua kutokana na mateso aliyokua anayapitia. Ukweli mateso aliyokua anapitia ukielezwa unaweza kutoa machozi. Siku hiyo aliamua kuchukua kisu na kuelekea porini kujimaliza kabisa ili aondoke duniani.

Alipofika sehemu ile aliyopanga kwenda kujiulia akakutana na kijana mwenzake anatokwa na machozi, akamsihi sana amweleze ni matatizo ambayo anayapitia kijana yule akaficha kisu chake mfukoni na akaanza kumsikiliza mwenzake. Alianza kusikiliza akafika mahali akaanza kutoa machozi kwa kusikia yale mwenzake ambayo alikua anapitia. Aliona kabisa yale anayopitia yeye sio mateso tena akaanza kumhurumia mwenzake. Mwenzake aliamua alikua ananyanyaswa na ndugu zake baada ya wazazi wake wote kuondoka duniani.

Alinyimwa kusoma na wala hakutakiwa kugusa chochote alichoachiwa na wazazi wake ukizingatia yeye ndio mtoto wa pekee na tayari alikua yupo kwenye umri wa kujitambua na alistahilia kupewa mali zake. Kijana yule alimwambia mwenzake anamshukuru Mungu kwa kua wamechukua mali zote lakini yeye wamemuacha hai. Na hapo alikua njiani kwenda mji wa mbali kuyaanza maisha yake mwenyewe akiwa hana ndugu wala binadamu yeyote anaemtegemea.

Akaenda mbali Zaidi kwa kusema kua wazazi wake waliuwawa kwa sumu hivyo baada yay eye kuigundua siri hiyo anatafutwa ili auwawe. Kwa hivyo yupo njiani kukimbia kuokoa maisha yake. Kijana yule aliekua anataka kujiua akaanza kujutia maamuzi yake ya kutaka kujiua kutokana na mateso kidogo aliyokua anayapitia. Akaamua kuongozana na kijana mwenzake waende kuyatafuta maisha yao wenyewe……….”

Inawezekana na wewe unapitia mateso ambayo unayaona ni makubwa sana, usikate tamaa Mungu ana sababu ya kukuweka hai endelea kuvumilia milango inakwenda kufunguka. Hatua ya kuchukua pale unapopitia mateso na shida ambazo unaziona ni kubwa sana tafuta mtu wa kumueleza kwani zinapokua ndani ya moyo wako zinakuchoma na kukuongezea maumivu. Tafuta mtu wa kuyasikiliza hayo unayopitia najua utaniambia Mungu yupo na anakuona na anasikia. Ndio usiache kumuomba Mungu Usiache kumweleza matatizo na mateso yako. Yeye ni mwema atakufungulia njia. Sikiliza pia wanayopitia wengine utajifunza kitu.

Usiwategemee wanadamu watakuumiza moyo mtegemee Mungu peke yake yeye yupo pamoja na wewe wakati wote kuna wakati utapitia magumu ukakosa wa kukusikiliza lakini ukiwa Mungu yeye atakufariji na kukutia moyo katika shida na mateso yako. Yeye anakupenda sana ndio maana kakuacha hai.

Embu tazama umeshamkosea mara ngapi lakini yeye anakusamehe anakulinda na ajali magonjwa ya hatari kama kansa na UKIMWI, yeye ni wa rehema sana yeye ndio yuko karibu yako zaidi kuliko mwanadamu. Anasema anakaa ndani yetu kama tukikubali na kumpokea.

Mruhusu aingie awe na wewe awe tiba ya matatizo yako. Ipo sababu yaw ewe kua hai leo haupo hai kwa bahati mbaya wengine wameuwawa kwenye vita, wengine wamefia kwenye ajali wewe sio mwema sana lakini ni sababu iliyokufanya wewe uwe hai.

Sababu hiyo unatakiwa uigundue mapema usiendelee kupoteza muda. Mungu amekuacha kwa sababu sio bahati mbaya wala nzuri. Mungu ana makusudi na wewe. Jitambue na anza kuzifanyia kazi sababu hizo.

Karibu sana.

#Siri_7_za_kuwa_hai_Leo.

#Jacob_Mushi_2016      

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading