UPO TAYARI KUACHA ALAMA GANI?

#SIRI_7
Siku moja nilijiuliza swali Nikiweza kutimiza ndoto yangu ya gari aina ya BMW X6 baada ya hapo nikaambiwa nimebakiza masaa machache nife  nitafurahia?

Nikajiuliza tena Nikiweza kutimiza ndoto yangu ya kujenga nyumba nzuri sana ya kuishi halafu nikaambiwa  bado siku mbili ufe je nitafurahia?
Nikasema tena na moyo Nikitimiza ndoto yangu ya kumuoa mke mzuri sana imetimia halafu nikaondoshwa duniani je nitafurahia?
Nikapata jibu kwamba yote hayo ukiyatimiza huwezi kuanza kufurahia ukifa bali utajuta.

Umeteseka sana miaka mingu ili ndoto yako itimie ya kumiliki vitu vizuri halafu unaondoka bila kuvifaidi.
Nikasema muda wangu hapa duniani nitautumia kufanya vitu ambavyo hata nikiondoka kesho nitaviacha bado vinaishi.
Kuwa na ndoto ya kumiliki gari zuri sio vibaya,  nyumba nzuri, kuoa au kuolewa sio vibaya. Ubaya unakuja pale ambapo hayo ndio mambo makuu kwenye maisha yako.  Huna jambo jingine unalolipigania libaki duniani.
Embu jiulize aliegundua mtandao unaotumia kusoma huu ujumbe yeye nyumba kwake ni nini? Gari nini? Anasa yeyote unayoijua wewe kwake ni ya gharama?
Hivyo vyote kwake ni vitu vidogo sana kwasababu aliwekeza kwenye kitu ambacho kinabaki daima. Hata akiondoka leo alichokianzisha kinabaki.
Kama ndoto yako kubwa sana ni kwa ajili yako mwenyewe hiyo ni ndoto ndogo sana.
JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA
#SIRI_7_ZA_KUWA_HAI_LEO
Jacob Mushi
www.jacobmushi.com
0654726668
This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *