Vile vitu vidogo vidogo unavyofanya na ukafanikiwa ndio vinakupa hamasa ya kufikika ushindi mkubwa. Kama utakuwa unadharau mambo madogo madogo ni rahisi kwamba huwezi kuyafikia makubwa.

Unawezaje sasa kuwa na ushindi mdogo? Siku zote ushindi mdogo huanza asubuhi na mapema. Ukifanikiwa kuamka mapema kabla ya wengine maana yake wewe ni mshindi. Umeshinda usingizi, umefanikiwa kuamka kabla ya wengine.

Kadiri unavyoamka mapema ndio unajitengenezea nafasi ya kufanya mambo mengi kwa ufanisi mkubwa Zaidi. Unajitengenezea nafasi ya kumaliza mipango yako ya siku mapema kuliko watu wengine.

Unapoamka mapema unakuwa na nguvu nyingi Zaidi kuliko aliechelewa kuamka. Unaweza kupangilia mambo yako kwa utaratibu mzuri. Ukichelewa kuamka unakuwa na haraka haraka na mwisho wa siku unaweza kuharibu kila unachokipanga.

Tatizo linakuja kwa wengi wanajiuliza nikiamka saa kumi kamili alfajiri nitakuwa nafanya nini? Mimi sina cha kufanya usiku wote huo. Mimi nimekuletea jibu la swali hilo, yapo mengi sana unaweza kuyafanya unapoamka mapema.

Siri ya kuamka mapema ni lazima pia ulale mapema. Kwa kawaida unatakiwa ulale masaa 7 hadi 8 yaani usingizi wa kukutosha. Kinachowafanya wengi wasilale mapema ni kwasababu wanakuwa bize na simu zao kabla ya kulala. Ili uamke saa kumi au kumi na moja alfajiri inatakiwa angalau saa nne na nusu uwe umeshazima data na upo kitandani umepumzika.

Unaweza kusema wewe una mambo mengi unafanya wakati huo. Na mimi nitakubaliana na wewe ila nitakuomba hayo mambo usiyafanye usiku huo bali yatengenezee muda wa kuyafanya asubuhi na mapema unapoamka.

Kuna mambo 3 ambayo ukiyafanya kila siku kwenye Maisha yako tena ukiyafanya asubuhi utakuwa na Maisha yenye mafanikio na ushindi kwenye kila unachokifanya. Mambo hayo utayapata ndani ya Programu yangu ya DAKIKA 20 ZA MAFANIKIO. Karibu sana ujiunge nami ili uweze kuianza siku yako kwa mafanikio makubwa.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/

Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading