Haijalishi unapitia hali gani sasa hivi wewe ni mshindi vita bado haijaisha mapambano bado hayajaisha endelea kupambana mpaka mwisho.

Haijalishi umelala njaa jana sio  mwisho wa mapambano endelea kupambana tafuta njia nyingine mpya lakini utazamie kufika mwisho uleule.

Haijalishi huna nini sasa hivi lakini bado inawezekana wewe kushinda nikupe moyo kwa yale unayoyapitia inawezekana ni mazito sana lakini usirudi nyuma.

Fursa zinakuja, milango itafunguka tu, njia utaanza kuziona muda sio mrefu usiache, pambana kwa njia yeyote ile.

Hata kama umevunjika moyo pambana vyovyote vile, haijalishi umeachwa na uliempenda bado sio mwisho wa mapambanao.

Haijalishi kwamba hakuna anaekusaidia, anaekutia moyo wote wamekaa pembeni wanakutazama pambana tu.

Hii vita ni yako, ni yako mwenyewe na lazima ushinde hakuna namna nyingine.

Haijalishi umevunjwa moyo kiasi gani, haijalishi umepata hasara kiasi gani bado sio mwisho wa pambano.

Hii ni vita juu ya ndoto zako na malengo yako usikubali kukata tamaa kirahisi hivyo unachokipigania ni cha thamani sana. Kitu chochote cha thamani kina gharama yake. Na hayo unayoyapitia sasa ndio gharama yenyewe.

Hauko mwenyewe unaepitia hayo wako wenzako pia maana kila mtu ana vita yake.
Haijalishi huna elimu kubwa lakini lazima ufanikiwe amua hivyo na anza kufanyia kazi ingia vitani sasa, vitani hakuna kurudi nyuma ni kushinda au kufa, sio kushindwa ondoa neon kushindwa katika akili yako na anza sasa mapambano.

Kwa sababu umezaliwa kwenye mazingira magumu haimaanishi kwamba utabakia kwenye mazingira magumu. Ni wakati wako wa kuamua kuanza kubadilisha hali uliyonayo sasa bila ya wewe kuamua kutoka ndani ya moyo wako hakuna kitakachobadilika.

Simama imara na amini kwamba mafanikio ni lazima kwako. Ushindi ni lazima kwako, haijalishi sasa hivi huna pesa, huna elimu, huna watu unaowajua, kinachotakiwa ni Imani kutoka ndani yako inayosema  “MIMI NI MSHINDI”
Wewe ni mshindi na ulizaliwa ili ushinde, wewe sio mtu wa kawaida haya yote hayatafanya kazi kama hayataanzia ndani yako amini hivyo na yafanyie kazi.
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading