USIBADILI TABIA KWA KUA UMRI WA KUOA/KUOLEWA UMEFIKA

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
USIBADILI TABIA KWA KUA UMRI WA KUOA/KUOLEWA UMEFIKA.
Habari ndugu msomaji wa mtandao huu. Karibu sana leo tunaenda kujifunza pamoja hii tabia yetu hasa vijana ambao tumefikia umri wa kupata mke na mume tumekua tukiambiwa “ukiendelea na tabia hii nani atakuoa/ utamuoa nani”
Ni ukweli hawajakosea kusema ila mimi ninakwambia leo ” usibadili tabia kwa sababu umefikia umri wa kuoa au kuolewa” kwanini nasema hivo sikwambii uendelee nayo ninataka uiache ila sababu iwe ni huitaki hiyo tabia.
Ninakuhakikishia kua ukiacha kiburi/dharau/umbea/ulevi/uhuni wa aina zote kwa kua tu umefikia kipindi unataka mke au mume hizo tabia utazirudia ukishampata unaemuhitaji. Hiyo ni kweli na iko wazii kabisa ndio maana ndoa zinavunjika. Sipo kwenye ndoa lakini nimefikiria kwa mapana zaidi. Acha tabia yeyote mbaya kwa sababu tu huitaki katika maisha unataka kua msafi na sio eti unataka kuoa au kuolewa.
Jiulize leo tabia uliyonayo ungependa mwanao aje kua nayo? Kama hapana bas badilika kua vile ungependa mwanao awe. Hapo utayafurahia maisha. Kama ilivyo kuzaliwa hadi umefikia hapo ulipo ni hatua mbalimbali  umepitia. Hivyo pia katika kuacha tabia uliyonayo ni hatua huwezi kuacha kwa siku moja. Itakuchukua muda mrefu lakini kadiri ya bidii na matamanio yako ya kuacha ndipo itakapoisha.
Unaweza kusema nimejaribu mara nyingi kuacha lakini nimeshindwa. Nakushauri fanya hivi.
1. Ziandike tabia zote mbaya kwenye notebook yako ( andika hivi mfano.: ninaacha ulevi)
2: Zisome kila siku na angalia ipi umeanza kuiacha
3: Ukiona bado zinakusumbua mtafute mtu unaemheshimu sana muelezee tabia inayokusumbua mwambie huitaki na unatamani kuicha atakusaidia na kukusimamia mpaka uiache. 
4: Nakushauri umpokee Yesu atakusaidia kukusafisha tabia zako zote maana damu yake yashinda yote ya ya dunia.
Asante sana kwa kusoma. Imeandikwa na
Jacob Mushi 0654726668 mushijcob@gmail.com
Karibu sana
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading