Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?
Ukweli ambao unaweza kuwa hupendi kuusikia ni huu, hakuna njia moja ambayo ni sahihi ukiifanya lazima ufanikiwe. Hakuna biashara ambayo ndio sahihi lazima ukiifanya ufanikiwe.
Kila biashara kuna waliofanikiwa Zaidi, wa kawaida na waliofeli na wengine wanajuta kabisa kufanya biashara hiyo. Hivyo rafiki yangu usikae mahali unasubiri biashara ambayo ukiifanya lazima ufanikiwe.
Wala asikudanganye mtu akakuhakikishia kwamba ukifanya biashara Fulani utafikia mafanikio. Chochote kinaweza kutokea hivyo badala ya kusubiria biashara nzuri ambayo ina mafanikio chagua kile unachokipenda kifanyie kazi jifunze kupitia makossa yako na utafikia kule unakotaka.
Tatizo la watu wengi ni kwamba hatupendi kujifunza, tunatamani kije kitu ambacho ukiweka juhudi kidogo unapata matokeo makubwa. Hatupendi kuweka bidi kwenye kazi zetu. Na ndio maana wengi tunadanganywa na kutapeliwa.
Hakuna kitu au biashara ambayo ni uhakika asilimia mia moja ukiifanya utafanikiwa. Hata matajiri wakubwa wanaingia kwenye biashara na kupata hasara kikubwa wanachoondoka nacho ni funzo. Wanajifunza ili wasirudie makossa waliyoyafanya mwanzo.
Kwa hiyo rafiki yako embu anza acha kutafuta kitu ambacho ni sahihi angalia wewe na mazingira yako mnahitaji nini kisha wanapatie. Chochote utakachokutana nacho njiani tafuta namna. Jifunze kile siku.
Rafiki Yako,
Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/
Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”
Nimependa sana nakala zako
Karibu sana Amani