Kuna watu huwa unaogopa kwasababu wanakufahamu kama mtu Fulani mkubwa hivi sasa unaogopa kufanya kazi ambazo unahisi kwamba zitakuwa zinakushushia hadhi?

Nilikuwa na rafiki yangu mmoja kipindi Fulani tukawa na wazo la biashara ambalo tulitaka kufanya pamoja. Mara nyingi yule rafiki yangu alikuwa anapenda kusema; “unajua biashara ukifanyia sehemu ambayo wewe ni mgeni ni rahisi sana kufanikiwa?”

Nami nikamuuliza “Kwanini unasema hivyo?”
Akajibu; “Unajua ukiwa sehemu ambayo wewe ni mgeni unakuwa na ujasiri Zaidi unaweza kuingia hata nyumba kwa nyumba ukauza bila woga”
Hapo nikamuelewa kwamba shida yake yeye ni watu ambao wanamfahamu anahisi hao watu walimuona nafanya biashara Fulani watasema ameishia, ameharibikiwa au maisha yake yamekuwa mabovu kabisa.
Hii shida tunayo watu wengi sana. 
Inawezekana hata wewe shida hii inakusumbua  unaogopa kufanya vitu Fulani kwasababu marafiki zako uliosoma nao chuo watakuona na watasema una hali ngumu.
Sasa nataka ujiulize swali, hivi wakisema una hali ngumu na ukweli ukawa ni hauna hali ngumu itakupunguzia nini? Wakisema maisha yako yako vizuri halafu mwenyewe unajijua hakuna pesa tena unatamani hata ungewakopa ina maana gani?
Hao unaowaogopa watasema maisha yamekushinda unapaswa kuwaweka kando. Hawana msaada wowote kwako kama kazi yao ni kukusema vibaya. 
Mtu yeyote anaepoteza muda wake kujadili maisha ya mwenzake hajui anachokifanya na bado hajaanza kuishi maisha yake.
Jiunge na Usiishie Njiani upate msaada pale unapokwama kwenye kile ulichoamua kufanya Jiandikishe hapa….. http://jacobmushi.com/jisajili-sasa/ 

Jipatie Vitabu vya Mafanikio na Biashara hapa…. http://jacobmushi.com/patavitabu/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading