Kitu chochote kinachopatikana haraka hasa kitu kikubwa sana mara nyingi yule anaekipata hushindwa kukihimili. Hasa tukiangalia upande wa fedha na utajiri tunaweza kuwa na mifano mingi sana ya watu ambao walipata fedha nyingi ndani ya muda mfupi na wakaishia kuwa maskini kama zamani. Unajua mafanikio ni sawa na mtu anaepanda juu kwenye kilele cha mlima. Sasa kama hujakomaa vizuri ukifika kwenye kilele utashindwa kusimama hasa wakati ukitazama chini unaweza kupata kizunguzungu.

Hatua za mafanikio haziitaji kwenda haraka endelea kupanda taratibu bila kujali kwamba umepitwa na wangapi. Hakuna unaeshindana nae usiogope kwa waliokupita. Endelea kuwekeza kwenye akili yako kwasababu ukishindwa hapo lazima utakwama kule unapoelekea.

Mafanikio ya kupanda mwendokasi siku zote huwa hayadumu kwasababu hakuna maumivu yeyote uliyopitia hapo katikati ili kukufanya uwe imara. Katika kabila la kimasai ili uweze kuonekana umekomaa kama mwanaume ilikuwa ni lazima uweze kumuua simba. Sasa kama hujaweza kumuua Simba utaonekana wa kawaida sana. Unajua kwanini simba? Simba ndio tatizo kubwa kwenye jamii yao. Simba alikuwa anakula mifugo yao pamoja na watoto wao mara nyingine. Hivyo unapoweza kupambana na simba unaonekana unaweza kubeba matatizo mengine.

Kama hujakomaa sawasawa lazima utaanguka. Hakikisha unaweza kutatua matatizo kwenye hatua uliyopo sasa hivi kwasababu yakikushinda hutaweza kuvuka hiyo hatua. Endelea kutatua changamoto kila changamoto unayoweza kutatua unakuwa umevuka na kupanda kiwango kingine.

Ukijenga mafanikio yako kwa namna ya kutatua matatizo hatua kwa hatua unajitengenezea msingi mzuri wa mafanikio makubwa Zaidi. Kadiri unavyopanda juu ndio matatizo ya kutatua yanaongezeka. Usifikiri unapokuwa mtu mkubwa basi ndio unakwenda kustarehe. Matatizo unayotatua yanakuwa ni mengin na makubwa kuliko mtu wa kawaida hivyo lazima ukubali kujijengea msingi mzuri kipindi hiki ukiwa huku chini.

“The greatest glory in living lies not in never falling, but in rising every time we

fall.” – Nelson Mandela

Nelson Mandela aliwahi kusema kuwa utukufu mkubwa haupatikani pale tunakuwa hatujaanguka bali ni pale tunaposimama kila tunapoanguka. Hivyo basi haijalishi changamoto gani unapitia ushindi wako upo pale unaposimama na kuendelea mbele. Hakuna kushinda kila wakati. Ukiona wewe unashinda kila wakati jua kuna mambo makubwa hujafanya bado. Hujafanya kitu kilichozidi uwezo wa akili yako.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading