#USIISHIE_NJIANI: ANZA KUONA NDANI YAKO.

Habari rafiki yangu,

Siku yako umeanzaj

Hakuna kitu utakachokipata kama hujaanza kukiona ndani yako. vitu vyote vinavyotokea nje lazima vinaanzia ndani.

Ukiwa na mawazo ya kupata pikipiki haliwezi kutokea gari, kwanza juhudi zako zote zitakuwa ni za pikipiki sio za gari. Usitegemee kupata Zaidi ya kile ulichokiona.

Ni vyema sana chochote unachotaka kufanya ukaanza kutengeneza picha ndani yako na sio kwa kuvutiwa na vitu wengine wanfanya au kwa kusikia hadithi za vitu vilivyoleta mafanikio ukavutiwa kuvifanya bila ya kutengeneza picha.

Kwa kuona ndani yako ndio utapata hamasa Zaidi kuliko kuona kwa wengine. Anza sasa kujenga picha kubwa ndani yako juu ya kile unachokifanya sasa hivi.

 

Amua leo unachokitaka na ujione ukiwa mbali kimafanikio. Kuna wengi wapo unaweza kujifunza kwao.

Yapo mengi yameandikwa unaweza kujifunza na ukafikia picha ulioiona ndani yako. Maisha yako ni kile unachokiona. Hivyo ulivyo sasa hivi ndio ulikuwa unaona miaka michache iliyopita.

 

Matokeo unayopata sasa hivi yanasababishwa na mtazamo uliokuwa nao miaka michache iliyopita. Badili mtazamo wako ili upata matokeo makubwa Zaidi ya sasa.

Tengeneza picha kubwa ili uanze safari ya kuifikia picha hiyo.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

 

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *