#USIISHIE_NJIANI: BINADAMU NDIVYO WALIVYO.

jacobmushi
2 Min Read

Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?

Kama utakumbuka ulipokuwa mtoto mdogo kuna mambo kutokana na utoto wako ulikuwa unapenda kujaribu sana. Kama ulikuwa mtundu sana, unaweza kupanda madirishani, mara umepanda juu ya mti. Unataka kuwasha taa, na mengine mengi. Kwa kawaida unapofanya jambo la tofauti wazazi au wakubwa zako watakwambia acha, utaumia, utaanguka, na wakati mwingine unaweza kuchapwa kwa kujaribu vitu.

Mara zote utaonekana wewe ni mtundu sana. Watoto watundu wanaonekana kama ni wabaya. Wazazi wako walitaka ukae tu usifanye chochote. Bahati mbaya watoto hawapendi kuonekana wao ni watoto. Wanataka kujaribu yale mambo ambayo mtu mzima anafanya.

Hawataki kuonekana wao hawawezi. Ndio maana akikuona unaendesha gari nay eye atataka ashike mstelingi. Akiona unalima na yeye anataka ashike jembe.

Sasa hata katika Maisha yako ya sasa hivi watu bado hawakuamini. Ndio maana ukiwaambiwa umemaliza masomo yako hutaki kazi unaenda kujiajiri wanaona kama utateseka sana. Bado wanakuchukulia kama yule mtoto mdogo anaetaka kujaribu kuendesha gari na kupanda madirishani.

 

Unapokuja na wazo zuri la biashara la tofauti wanakwambia haiwezekana haijawahi kutokea. Hivyo usiwaogope. Usikatishwe tamaa na maoni yao. Ni kwasababu tu wanakuchukulia kama mtoto mdogo ndio maana hwataki ujaribu vitu vipya. Wanatamani uwe kama wao. Uishi Maisha ambayo watu wengi wamezoea kuishi.

Waelewe ndivyo walivyo binadamu endelea mbele. Hakuna wa kukuchapa tena.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading