Leo jioni nikiwa nazishika ndevu zangu ghafla katika fikra yakanijia maneno ambayo niliambiwa miaka karibia kumi iliyopita. Kuna mtu mmoja aliniambia “wewe ukiwa na ndevu utakuwa mbaya sana”.

Nikabaki najiuliza kwanini haya maneno yamekuja sasa hivi wakati nashika ndevu? Mbona ni muda mrefu sana umepita na nilishayasahau kabisa? Nikagundua kwamba maneno uliyonenewa na watu yanabaki ndani ya moyo wako.

Unaweza kukuta kuna mambo hayaendi kwenye maisha yako sasa hivi kumbe kuna maneno ulishanenewa kipindi cha nyuma na yanautesa ufahamu wako. Kama kuna mtu alishwakwambia wewe una sura mbaya na hujawahi kuyakataa hayo maneno yataendelea kukutesa. Huwezi kujikubali hata siku moja. Utajikuta unakosa ujasiri ukisimama mbele watu.

Kama kuna mtu alishakwambia kwenu mna mikosi basi utajikuta kila unalofanya linaharibika kwasababu ya yale maneno uliyonenewa.

Akili yako imekuwa inajengeka kutokana na maneo uliyokuwa unaambiwa tangu ukiwa mtoto. Hivyo kila unalolifanya linakuwa linatokana na yale uliyoambiwa.

Usikubali maneno haya yaendelee kutesa maisha yako. Una uwezo wa kuyafuta kabisa kwenye maisha yako. Una nguvu ya kujenga upya kile unachotaka kitokee tena ndani ya maisha yako.

Amua kuanzia sasa uandike yale mambo unayotaka yatokee kwenye maisha yako na uwe unayasema. Unapoyasema unafuta maneno mabaya uliyowahi kuambiwa hata kama ulishayasahau.

Fanya zoezi hili mara kwa mara utaanza kuona matokeo yake.

Usiendelee kuishi kwenye maneno ya watu ambayo yalinenwa juu yako miaka iliyopita. Una nguvu ndani yako ya kukuwezesha kuishi yale maisha unayotaka.

Kata kuwa mtumwa wa maneno yaliyoumbwa juu yako.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading