Habari rafiki, siku yako umeanzaje.

Siku zote mtu anakosa ujasiri hasa pale anapokuwa na taarifa chache kwenye kile anachokifanya. Mfano unaweza kuogopa kuanza biashara kwasababu tu ya kutofahamu mambo ya muhimu juu ya  biashara.

Ili uweze kuishinda hofu hii unapaswa kujifunza vitu Zaidi kwenye kile ulichoamua kukifanya. Hii itakusaidia wewe kuwa na taarifa za kutosha na kuongeza kujiamini kwako.

Mara nyingi hofu hii imewafanya watu wakabaki vile walivyo na kuogopa kujaribu chochote kwa hofu ya kushindwa. Usikubali kubaki hivyo ulivyo kwasababu tu hujui kitu Fulani, uliza maswali na utapata majibu.

Chukua hatua mambo mengi utajifunza na kuyafahamu Zaidi wakati ukiwa unafanya. Usisubiri kujua kila kitu ndipo uanze anza vingine utajifunzia mbele, hauendi kushindana na mtu kwamba atakushinda unashindana na malengo yako na ndoto zako.

Unachopambana ni kutimiza ndoto zako hivyo usiogope kwamba watu watakuonaje. Ingia anza achana na hofu hii ya kutokujua. Usikubali ikufanye ubaki hapo ulipo siku zote.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading