Habari Rafiki. Chochote unachokifanya sasa hivi kabla hujaanza kukata tamaa hakikisha umejipa muda wa kutosha. Jipe muda ambao utafanya kazi kwa bidi, utajenga mtandao mkubwa wa watu wanaofahamu unachokifanya. Jipe muda wa kujifunza na kuona kule unakotaka kufika.

Shida kubwa ipo kwa watu wasio na maono makubwa wanataka pesa za haraka. Unaanza biashara au wazo lako mwezi uliopita unataka uanze kuona hela. Ndugu yangu kubali kujipa muda. Kubali kutoa Zaidi kwanza. Toa vya kutosha halafu vitaanza kurudi.

 

Jipe muda wa kujifunza kama kweli unataka kufika mbali lazima utoe muda ambao utajifunza sana biashara yako na kujua ni wapi hasa pa kuweka nguvu Zaidi. Kadiri unavyokuwa ndivyo wazo lako linazidi kupanuka na kuongezeka ukubwa. Usipojifunza hutajua ni vitu gani ufanye ili kuleta mabadiliko. Fursa nyingi utaziona ndani yaw azo lako kadiri linavyokua fursa hizi zinaweza kuwa ni mpya kabisa na hukuwahi kuzifikiria wakati unaanza.

 

Jipe muda kwani mabadiliko yanakuja kila siku kile unahcokiona kigumu leo huwezi jua kesho kitakuwa kimerahisishwa kama utakata tamaa walioendelea kukomaa watafaidi mabadiliko. Ni kweli kuna nyakati ambazo unakutana na ugumu wa kutisha kiasi kwamba unaona giza. Huu ndio wakati unapaswa kujua umuhimu wa kuwa na mentor mtu ambaye anayafahamu vyema maono yako. atakushauri pale usipoweza kuona mbele.

 

Usidanganywe na mtu anaetaka hela za haraka haraka. Watu wengi nimekutana nao wanataka kufanya biashara ambazo leo na kesho ataanza kupiga hela. Ni biashara nzuri sana za hivyo lakini ni mara chache zinadumu. Na hii ni kwasababu unakuta hazina msingi imara. Hakuna sehemu ngumu kama kujenga msingi. Na hakuna sehemu nzuri ya kufurahia kama kuwepo kwenye nyumba iliyokamilika na yenye msingi imara unakuwa huna hofu.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading