Unavyoanza siku yako ndivyo inakwenda kuwa siku nzima. Kama ulianza kwa kugombana na wengine basi ujue siku yako yote itakuwa ni ya kukosana na wengine.
Inawezekana umekuwa unasema hii siku imekuwa na mikosi kumbe ni wewe mwenyewe ulianza vibaya siku yako. Inawezekana ukalalamika na kuona siku imekuendea vibaya kumbe ni namna ambavyo ulianza bila ya kujiandaa.
Usikubali kuanza siku yako kienyeji utaipoteza lazima uwe na utaratibu wa kujiandaa unapoanza siku ili kupata mafanikio makubwa.
Leo nakwenda kukupa maneno au kauli au tunaweza kusema misemo ambayo unapaswa kujisemesha kabla hujaenda popote yaani ukiwa ndani kwako kabla hujatoka nje.
Leo ni siku mpya nakwenda kupata matokeo mapya Zaidi ya jana.
Kila siku ni mpya, kila siku inakuja na Baraka zake lakini unapaswa uanze kuziteka Baraka hizo kwa kujitamkia. Jitamkie kwamba unakwenda kupata Baraka za siku hiyo mpya kwenye kila utakachokwenda kufanya.
Kila nitakachokigusa Leo kitaniletea Matokeo Makubwa.
Jiambie kwamba kila unachokwenda kugusa na mikono yako, iwe ni bidhaa basi utauza sana, kama ni kazi itakuwa bora kuliko siku zingine.
Mimi ni Mshindi Nakwenda kuzishinda changamoto zote.
Ndio changamoto zitakuja lakini unaanza kuziandalia ushindi mapema asubuhi. Kwa kusema hivyo unaindaa akili yako iweze kukupatia majibu ya changamoto zote utakazokutana nazo siku ya leo.
 
Soma: Sio Kwamba Huwezi
Nakwenda Kujaribu tena pale nilipokwama jana ili Nishinde.
Jana inawezekana umejaribu vitu mbalimbali na ukakwama au ukashindwa kukamilisha leo ni siku nyingine mpya kwenda kukamilisha yote ulikwama jana.
Nakwenda kuwa na siku ya furaha na Ushindi leo.
Ndio siku yako yote ya leo inakwenda kuwa ya ushindi na furaha kwasababu umejiandaa vyema.
Hakikisha unazipitia ndoto zako kubwa ili kuongeza hamasa Zaidi, pitia malengo yako ya wiki nzima na ya siku husika. Kama hukuweka malengo ya siku ya leo basi wakati huu wa asubuhi ndio wa kuandika mipango yako ya leo. Kauli zote hizo hazina maana kwako kama hakuna kitu unachokwenda kufanya kama hauna malengo unayotaka kutimiza ni sawa na unapoteza muda kujisemesha.

Jifunze na Ufanikiwe kwenye Ujasiriamali, na Biashara.
Tambua Kusudi la wewe kuwa Hai Ufanikiwe.

Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading