Kwa lolote lile ambalo unapitia kwenye maisha yako sasa hivi. Liwe zuri au liwe baya ni vyema kuwa na muda wa kujiuliza swali kwa yote hayo unayopitia ni yapi unajifunza?

Kwa yote yanayoendelea kwenye maisha yako ni somo gani unaondoka nalo? Usikubali tu kuishia kuumia au kufurahi bila kuondoka na somo lolote.

Ukiwa mtu ambaye hamna unachojifunza kwenye maisha unayoishi kila siku unakuwa mmoja wa watu wa ajabu sana waliowahi kutokea hapa duniani.

“Intelligent individuals learn from everything and everyone; average people, from their experiences. The stupid already have all the answers.”
― Socrates

Mwanafalsafa Socrates wa miaka mingi sana iliyopita aliwahi kusema,” watu makini wanajifunza kwenye kila kitu na kwa kila mtu, watu wa kawaida wanajifunza kutokana na uzoefu wao, watu wapumbavu tayari wana majibu ya kila kitu.”

Ukishaona wewe una jibu la kila jambo na unajiona una hekima kuliko wengine. Una majibu na sababu za kutosha kwanini uendelee kubakia hivyo ulivyo. Una dharau mafundisho unaingia kwneye kundi la watu hawa wa mwisho ambao ni wapumbavu.

Hii ni msemo wa miaka ya zamani sana lakini tukiangalia katika maisha yetu ya kila siku hawa watu wapo. Hawa watu ambao wanajifunza kwenye kila kitu na kwa watu wote tunao. Watu wanaofikiri wao wanajua kila kitu pia tunao.

Kuna watu watu ukiwaambia mitandao ya kijamii inapoteza muda atakwambia kwani ilitengenezwa ili iweje. Haiwezekani wote tukawa matajiri, na majibu mengine mengi ambayo yanaoonyesha kabisa mtu huyu anafikiri anajua kila kitu na ana majibu ya kila kitu. Usikubali kuwa mpumbavu pedna kujifunza kwa kila linalotokea kwenye maisha.

Usikubali kuwa katika kundi la wapumbavu kuwa katika kundi la watu ambao wanajifunza kwa kila linaloendelea kwenye maisha. Kama kuna mtu anafanya makossa mahali basi kuna somo la kujifunza hapo. Kama kuna mtu anafanya vizuri mahali pia kuna somo la kujifunza kwake.

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading