#USIISHIE_NJIANI: KUWA MTU WA SHUKURANI.

Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?

Pamoja na hali uliyonayo sasa hivi yaani hujafikia malengo yako kwa kiasi kikubwa bado una mengi ya kumshukuru Mungu. Embu watazame wasio na uwezo kama wako, watazame wanaokosa kula lakini wewe hujakosa mlo hata mara moja.

Watazame wanaokosa maarifa kama haya, hawajui wafanye nini, hawana mtu wa kuwashauri. Watazame walioko sehemu yenye vita na machafuko hawana mawazo yeyote juu ya Maisha yao ya baadae wao wamekuwa ni kukimbia kimbia tu.

Ukweli una mengi ya kumshukuru Mungu. Unapojitengenezea moyo wa shukurani kwa kila jema ambalo unalipata kwenye Maisha yako unajitengenezea nafasi ya kupata mema mengi Zaidi.

Wako wenye mahusiano mabovu kila kukicha ni kugombana wewe ndoa yako ina Amani embu mshukuru Mungu. Kuna ambao wanatafuta cha kufanya hawapati wewe tayari unacho kitu kinakuingizia kipato.

 

Maisha yako yatakuwa yenye furaha sana kama utakuwa ni mtu ambaye ana shukurani. Embu jitazame ulipotoka na sasa upo wapi utaona mengi ambayo yanapasa kusema asante kwa Mungu.

Ukiwa mtu wa shukrani unajiepusha na lawama, sababu, na kujitetea. Watu wengi wasio na shukurani huwa watu wanaolalamika siku zote. Hivyo acha kuwa upande njoo upande wa shukrani. Ukiwa unashukuru kwa kidogo mambo makubwa Zaidi yanafunguka mbele yako.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading