Habari rafiki, umeanzaje siku yako. Leo ni siku yetu mpya kwa ajili ya uzalishaji. Kuna watu wana tabia za kuacha kufanya mambo yao, hawaweki mipango yeyote ya Maisha yao wanabaki kusema lolote linaweza kutokea.

Umemaliza chuo badala a kungoja lolote linaloweza kutokea ndio likupangie Maisha yako yaende vipi anza kujipanga mwenyewe mapema.

Hakuna lolote linaloweza kutokea na halijapangwa. Kama hukujiandaa usifikiri kuna mtu tu atatokea huko akuitie kazi.

Badala ya kusubiri muujiza nenda kwenye majukumu yako ya kila siku muujiza ukukute njiani. Usingojee muuujiza ukiwa umekaa ndani.

 

Jua unapokwenda acha kupoteza muda.

Hilo unalodhani kwamba linaweza kutokea mara nyingi halipo n ahata kama lipo haliwezi kubadili Maisha yako kwa kiasi kikubwa kama lingetoka ndani yako.

Hata zile ajira za kushangaa umepigiwa simu unaitwa kwenye usaili siku hizi ni chache sana. Ni vyema ukajipanga mwenye mapema badala ya kusubiria lolote linaloweza kutokea.

 

Kuna watu ukiwauliza miaka mitano ijayo utakuwa wapi wapi wanakwambia “unajua tunapanga lakini na MUNGU anapanga. Unaweza ukapanga lakini lisitokee hata limoja” acha ujinga unajua Mungu amemwambia Yeremia unaona nini? Unajua yeye ndie alimwambia aandike kile anachokiona. Sisi tunapanga ndio lakini ukiwa nje ya kusudi lake ndio mambo yako yataharibika.

Sidhani kama kusudi la Mungu ni wewe uwe na Maisha ya kimaskini.

Weka mipango ndugu yangu ya Maisha yako, acha kusubiria usichokijua.

 

UFANYEJE SASA:

Jua mwelekeo wa Maisha yako.

Kuwa na maono makubwa ambayo unayafuata kila siku.

Fanyia kazi maono yako kila siku.

Fanyia kazi maono yako kila siku.

Narudia tena fanyia kazi maono yako kila siku.

Hilo lolote likija likukute kwenye kazi, likukute kwenye mwelekeo wako unaoeleweka.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading