#USIISHIE_NJIANI: MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIISHIE NJIANI.

jacobmushi
3 Min Read

Furahia kila wakati unaopitia lakini usijisahau kuwa upo safarini. Unapokuwa safarini tena kwenye safari hii ya maisha kuna mengi utakutana nayo njiani usikubali kubakia sehemu moja kwasababu kuna mazuri umekutana nayo. Furahia hayo mazuri lakini usikubali yawe sababu ya wewe kubakia hapo.

Kwenye maisha jifunze kuchagua kwani kile unachochagua kinaonyesha jinsi wewe ulivyo. Marafiki ulionao, namna unavyovaa, unavyoongea vyote vinakutambulisha wewe. Jifunze kuchagua vyema kwani vile ulivyochagua vinaelezea moyo wako ulivyo.

Watu waliokuzunguka wana mchango gani kwenye safari yako? Kumbuka kuwaepuka aina ya watu ambao wakija kwenye maisha yako wanataka wakufaidi pekee. Ukishaishiwa wanakukimbia tengeneza aina ya watu ambao mtaweza kusaidiana sehemu mbalimbali na sio mmoja kumnyonya mwingine.

Kaa mbali na watu wanaotaka ufuate ratiba zao lakini kamwe hawataki kuhusika kwenye mambo yako. Usimpe mtu ruhusa ya kukuendeshea maisha yako na kukufanyia maamuzi yeyote. Wape watu nafasi ya kukushauri na sio kukufanyia maamuzi. Hii ni kwasababu lolote litakalotokea kwenye maisha yako wewe ndiwe utahusika. Hasa yanapotokea mabaya utalaumiwa wewe na sio hao wanakufanyia maamuzi.

Ishi maisha yenye malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Hii itakusaidia kupata mwelekeo wa maisha. Usikubali kuridhika na hicho ulichonacho endelea kuweka malengo makubwa Zaidi ya hapo ulipofikia. Haijalishi unapata kila unachotaka jua kwamba kadiri unavyokuwa na vingi unakuwa na uwezo wa kuwasaidia wengi Zaidi.

Mtoto mdogo akisema kutambaa ni kuzuri sana halafu akasema ngoja mimi nibaki hapa hapa niwe natambaa, kwakweli hawezi kuishi vyema hapa duniani. Kuna maisha ili uweze kuyaishi lazima uwe umevuka hatua Fulani. Huwezi kuogelea vizuri kama hujajua kutembea vizuri.

Kuna vitu ili uweze kubeba lazima uwe umekomaa. Na ili ukomae lazima upitie kwenye mambo yatakayoweza kukukomaza. Huwezi kujua uwezo wako wa kutatua matatizo kama hakuna matatizo yeyote unayopitia kwenye maisha yako. Usiogope changamoto unazopitia wewe songa mbele kila siku.

Maisha yako ni somo kwa wengine hivyo usikubali kukata tamaa kuna watu watakuja kujifunza kwenye maisha yako. Kuna watu wanataweza kufanya makubwa kwasababu unawaandalia njia sasa hivi.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. jacobmushi.com/vitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. netpoa.com

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading