Ili uweze kupata chochote unachokitaka lazima uanze kuona kwenye akili yako kabla hakijatokea kwenye uhalisia. Anza kutengeneza picha ndani ya fikra zako ndipo utaweza kupata kwenye uhalisia.

Hakuna kitu kinatokea chenyewe kwenye maisha yako kama ajali lazima uanze kutengeneza picha na uifanyie kazi picha hadi itokee.

Unajua muujiza unatokea bila ya sisi kutarajia au pale tunapokuwa tumekata tamaa kabisa lakini ukweli ni kwamba kunakuwa na mchakato unaofanya muujiza utokee.

Na mchakato huo lazima uhusike wewe mlengwa wa muujiza. Haiwezekani ukapokea uponyaji wakati bado hujaanza kuamini ndani yako. Lazima kwanza uamini na uchukue hatua za Imani ili muujiza utokee.

 

Kama muujiza wenyewe unaanzia ndani yako vipi kuhusu yale unayoyataka? Je yale maisha mazuri unayosemaga lakini huwezi hata kuyaelezea unafikiri yanatokeaji?

Ili upokee lazima ujue unachokitaka, Barthimayo kipofu alipiga kelele barabarani akimwita Yesu mwana wa Daudi. Msafara ukasimama Yesu akamfuata alijua kabisa huyu mtu ni kipofu na shida yake ni kupona lakini alimuuliza wataka nikufanyie nini? Hii inaonyesha kwamba lazima ujue unachokitaka ndipo upewe.

Kujua unachokitaka ni hatua ya kwanza kabisa kwenye maisha yetu. Watu wengi sana hawajui ni nini hasa wanataka kwenye maisha. Wengi wanaishi maishaya kuiga kwasababu Fulani amefanya vile na wewe unataka.

 

Lazima ujue ni nini hasa unataka maishani mwako na uanza kufanyia kazi hatua kwa hatua hadi vitokee.

Yaone maisha yako vile unavyotaka yawe ndani ya ufahamu wako kabla hujafikia kwenye uhalisia. Usiogope hali uliyonayo sasa isikutishe kuona mambo makubwa.

Tengeneza picha kubwa ambayo itakuamsha asubuhi na mapema kwenda kuifanyia kazi ili itimie. Tengeneza picha kubwa ambayo itakusukuma uifanyie kazi usiku na mchana hadi ije kwenye uhalisia.

ONA VITU KABLA HAVIJAYOKEA.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading