#USIISHIE_NJIANI: UNATAKA KUJA KUWA NANI?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Habari za Asubuhi Rafiki. Hili swali kama unakumbuka ulikuwa unaulizwa ukiwa mdogo. Na mara nyingi watu wengi walikuwa wanachagua vitu ambavyo wataweza kuvisomea chou kikuu. Sasa makossa uliyokuwa unayafanya bila ya kujua ni kwamba ulisahau kuna vitu vingi ambavyo ungeweza kuwa hata bila ya kuvisomea shule. Kama unakumbuka ni wachache sana walikuwa wanachagua kuwa matajiri.

Kama unakumbuka ukichagua vitu ambavyo huwezi kusomea ulikuwa unagombezwa ili uchague vizuri, mfano ukisema unataka kuja kuwa mchezaji, au mwanamuziki ulikuwa unaonekana umechagua kitu ambacho hakina maana sana. Lakini kwa sasa tunaona vipaji vilivyoweza kuwatoa wengi tena wakiwa bado vijana wadogo.

Sasa leo napenda kuchukua nafasi hii kukuuliza tena swali lile lilea ulilokuwa unaulizwa ukiwa mtoto  UNAPENDA KUJA KUWA NANI? Je unapenda jamii na watu wote unaokutana nao wakutambue kama nani? Haijalishi umesoma au haujasoma hapa unatakiwa ufikiri tena upya.

 

Hili swali unapaswa kujiuliza mara kwa mara kwasababu linakupa picha ya kule unakotaka kwenda. Linakufanya utengeneze mwelekeo wa Maisha yako. kama hujitambui unataka kuja kuwa nani basi unapoteza muda mwingi hapa duniani. Hata vitu unavyovifanya hujui kwanini unavifanya.

Jiulize swali hili mara kwa mara hasa pale unapotakiwa kufanya maamuzi ya mambo kwenye Maisha yako. umekuja hapa duniani ili kulitimiza lile kusudi lako kuishi kwako. Kama utashindwa kutambua kusudi hilo basi ni vyema sana ukajiuliza maswali mara kwa mara.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading