Habari rafik Mfano unajua kabisa yale ambayo unayafanya hayawezi kukuletea matokeo ya tofauti kwasababu ni yaleyale, njia ni zilezile, halafu unajitia moyo kwamba ipo siku utafanikiwa.

Unajua kabisa unaogopa kufanya vitu vipya, husomi vitabu, hujaongeza chochote kwenye akili yako halafu unasema ipo siku yatatokeo, huo ni uongo, unajidanganya mwenyewe. Angalia matendo yako ya jana kama yanafanana na leo matokeo yatakuwa ni yaleyale.

Kila siku kuna mabadiliko yanatokea hujaamua kujiongeza uone ni namna gani utajifunza ili uendane na mabadiliko hayo, lakini bado unajitia moyo tu ipo siku. Wakati mwingine unatakiwa ujitazame uone ni wapi unajidanganya na ni wapi unafanya kweli.

Kwa kawaida mwanadamu anapenda kutiwa moyo, kusifiwa, kuambiwa amefanya vizuri hata kama amekosea. Ndio maana ukiwa mtoto ukigombezwa unaweza kulia lakini ukweli ndio huo. Unapokosea kubali kwamba hapa nimeharibu aisee. Unapofanya mambo ya kawaida kubali hapa hakuna kipya nilichofanya.

 

Mara nyingi penda kukaa peke yako zitazame kazi zako unazofanya na jinsi unavyozifanya, utaona kuna makossa wapi na wapi huwa unafanya makossa.

Baada ya kugundua unapokosea sasa usibaki chini ukijilaumu. Anza kubadilika, rekebisha kule unapoona kabisa hapa nimeboronga. Hapa bado sijaweka nguvu za kutosha.

 

Na hapo ndipo utaanza kuona matokeo makubwa kwenye kile unachokifanya. Kama kuna sehemu umekuwa unazembea acha uzembe sasa. Kama kuna sehemu umekuwa unafanya kwa mazoea acha mazoea. Nenda hatua ya ziada.

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading