Habari ya asubuhi Mwanamafanikio. Tumeanza tena wiki siku ya leo. Hakikisha umeipanga wiki yako ili uweze kuwa na matokeo bora. Jua ni vitu gani unakwenda kukamilisha wiki hii kbala haijaanza panga ratiba zako vizuri la sivyo watu wengine watakuja na ratiba zao na wewe utaingia humo. Mwisho wa siku mambo yako yanakuwa hayaendi.
Nadhani kila mmoja amewahi kusikia ofa imetangazwa kisha mwishoni wanasema vigezo na masharti huzingatiwa. Ni kweli kabisa kama hujatimiza vigezo vya kupata ofa iliyotangazwa huwezi kupata ofa.
Sasa na mafanikio nayo yana vigezo vyake na masharti, kuna vitu usipovifanya au ukizembea unaweza kujikuta unazunguka pale pale siku zote. Halafu ukaanza kumtafuta mchawi ni nani.
Kwenye mahusiano kila mtu anapofikia kuchagua anakuwa na vigezo vyake na masharti yake. Sasa unaweza ukafikiri wewe una vigezo vyote vya kuolewa kama binti labda una sura nzuri, una umbo zuri ambalo kila mtu anatamani kuwa na wewe. Lakini ukisahau kwamba kuna vigezo na masharti ambavyo unatakiwa uwe navyo Zaidi ya hivyo vinavyonekana kwa nje utakikuta unaishia kuchezewa na kuachwa.
Unapokwenda dukani kuchagua nguo huchagui tu kwasababu ni nzuri lazima uwe na vigezo. Lazima uchague nguo inayokutosha. Lazima uchague nguo kulingana na tukio unalotaka kwenda kuvalia. Lazima uchague nguo inayoendana na maadili yako unayosimamia.
Sasa ukifiikiri wewe ni mzuri utachaguliwa tu utaishia kushikwa na kila mteja anaekuja kisha unarukwa. Kumbe tatizo halipo kwenye uzuri wako tatizo lipo kwenye vigezo vya wachaguaji. Tatizo lipo kwenye aina ya mtu uliejitengeneza. Tabia zako ndio zinaamua Maisha unayoishi pia fursa na changamoto unazopitia.
Kabla hujalalamika kwanini hupati kile unachokitaka jiulize umefikia vigezo na masharti? Kama hujafikia vigezo na masharti endelea kujiboresha.
Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/
Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”