Mti unapokuwa kwenye mazingira ambayo hayasababishi mti usitawi unakuwa hauna namna yeyote ya kubadilisha mazingira yale ili uendelee kukua. Mara nyingi kinachotokea baada ya mti kuwepo sehemu ambayo haina rutuba na pia haina maji ni kukauka au kupambana na hali hiyo mwishoe ni kudumaa.

Sasa wewe rafiki yangu sio mti, kama mazingira uliyopo yanakunyima fursa za kukua kwanini unang’ang’ania hapo? Kwanini unakubali kuendelea kudumaa?

Una uwezo, una nguvu, una akili, na una kila namna ya kukuwezesha kuchagua ni wapi uishi ili uendelee kukua. Kuendelea kubaki sehemu halafu unayalaumu mazingira unakuwa umekosa namna ya kutumia ufahamu wako vizuri.

Mti pekee ndio unaweza kuyalalamikia mazingira yamesababisha ukashindwa kukua. Binadamu amepewa uwezo wa kuamua na kuchagua mahali pa kuishi.

Kama sehemu uliyopo inakunyima fursa za kuendelea, badilisha mazingira hayo yawe vile unavyotaka. Kama huwezi kuyabadilisha ondoka hapo nenda sehemu nyingine.

Siku zote vitu ambavyo hatuwezi kuvibadilisha tusipokuwa makini huwa vinatubadilsha sisi. Mojawapo ya vitu hivyo ni mazingira. Ukishindwa kuyafanya mazingira yawe vile unavyotaka wewe, yatakufanya uwe vile yalivyo.

Mti unapokuwa sehemu ambayo haina maji ya kutosha na rutuba ndogo huishia kudumaa. Mwanadamu vilevile anapokuwa sehemu ambayo haina msaada wa yeye kuendelea mbele mara nyingi huishia njiani. Hukata tamaa kwenye ndoto zake. Huwa na ufahamu uliojifunga yaani unaona kama ndio haiwezekani tena lakini kumbe wewe sio mti wewe ni mtu.

Unayo kila sababu ya kufanikiwa.

Unao kila uwezo wa kufanikiwa.

Unazo nafasi za kufika juu kabisa kwenye mafanikio.

Wewe umechagua nini? Ukichagua kutafuta sababu kwanini huwezi hutaweza kabisa. Ukitafuta sababu kwanini unaweza, na namna ya kutoka hapo ulipo utazipata.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading