Home » MAFANIKIO MAKUBWA » 453; #USIISHIENJIANI LEO: Kufikiri, Unavyoishi, Unavyokula.

453; #USIISHIENJIANI LEO: Kufikiri, Unavyoishi, Unavyokula.

“The way you think, the way you behave, the way you eat, can influence your life by 30 to 50 years.” -Deepak Chopra


Vile Unavyofikiri, unavyotenda na kula, ina nguvu sana katika maisha yako ya baadae. Afya yako miaka 30 ijayo itatokana na kile unachokula sasa hivi.Maisha Yako kwa ujumla yanatengenezwa na fikra zako. Vile unavyojiona, Unavyofikiri juu ya fedha, Mahusiano, jamii ndio itaamua uweje miaka 50 ijayo.


Tabia Zako unazotenda kila siku ndio zinaamua uje kuwa mtu wa aina gani. Rafiki huu ndio ukweli hakuna kitu kinatoka nje yako wewe.
Maisha Yako kwa asilimia kubwa yanatengenezwa na vile unavyokula, unavyofikiri na unavyotenda.


Anza kujihusisha na kula yako, fikra zako na tabia zako ili uweze kubadilisha maisha yako. Chochote unachoweka ndani yako ndio kinaleta matokeo.


AFYA, HEKIMA NA UTAJIRI. Vile unavyokula, Vile Unavyofikiri, Vile Unavyofanya.


Maisha Yako yapo mikononi mwako. Chukua Hatua Sasa.


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi

About

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: