“No one loves the man whom he fears.” -Aristotle
Hakuna anaempenda mtu anaemuogopa.
Kuna tofauti kubwa ya mtu kukupenda na mtu kukuogopa.

Mtu akikuogopa anaweza kufanya kila unachotaka afanye na wewe ukafikiri anakupenda kumbe anakuogopa.

Usiwafanye watoto wako wakuogope ili wasifanye yale ambayo hutaki. Watafanya tu wakati wakijua haupo au huwezi kujua. Wakikupenda watakutii na kukusikiliza.

Watu unaowaongoza hupaswi kuwatisha ili wakuogope kwasababu watafanya kazi kwa bidii mbele yako lakini unapoondoka wataendelea kutegea.

Upendo ndio una nguvu pekee ya kumsukuma mtu kufanya jambo mwenyewe bila ya kulazimishwa.

Hakikisha siku zote watu wanafurahia uwepo wako kwasababu hicho ndio kitu cha pekee kinachowafanya wakutii hata usipokuwepo.

Kuogopwa sio heshima, Kupendwa ndio heshima. Ukiona unaogopwa ujue wewe ndio uko kwenye matatizo kwasababu utakuwa na wanafiki wengi nyuma yako.

Watu Wakikupenda watafanya kila kitu kwa moyo na wala sio kwa hofu.

Kuogopwa na Kupendwa ipo kwenye kila sekta, familia, Mahusiano, Kazini, uongozi, Siasa.

Kumbuka chochote Unachokifanya kwa hofu kuna Uwezekano mkubwa wa kukosea kwasababu msukumo sio kufanya kazi nzuri bali hofu ya yule anaekusukuma ufanye.

Vilevile watu wakikuhofu watashindwa kuwa na ukaribu na wewe. Watashindwa kujieleza kwako vizuri. Watashindwa kusema yale wanayopitia.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading